MTOTO WA MCHUNGAJI MHE.JOSHUA NASSARI HATIMAE NDOTO YAKE YAKUINGIA MJENGONI DODOMA YATIMIA.
Siku Za Nyuma niliwahi ona Maono kuwa nimekuwa Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, na ndoto hii imekuwa ikinisumbua mno, nilipokuwa nashiriki nilijua nitashinda na hata mwaka 2010 nilijua nitashinda lakini CCM walichakachua matokeo, ninajua Haki ya Mtu huwa haipotei ila inacheleweshwa, kwa sasa Namshukuru Mungu Kwa Ushindi huu, leo ndoto yangu imetimia". Maneno hayo yamesemwa na Mbunge Mchaguliwa katika Jimbo la Arumeru Mashariki Mh.Joshua Nassari
Mh.Joshua Nassari Mbuge wa Arumeru Mashariki.
Akitangaza matokeo hayo ya uchaguzi msimamizi wa uchaguzi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Wilaya ya Arumeru, Gracias Kagenzi, alisema kuwa Mgombea Ubunge wa Joshua Nassari CHADEMA amepata jumla ya kura 32,972, na huku mpinzani wake mkubwa, Sioi Sumari wa Chama cha Mapinduzi (CCM) akipata jumla ya kura 26,757.
Mpinzani wake alikuwa akichuana nae Bwana Siosi Sumari wa Chama cha Mapinduzi.
Mpinzani wake alikuwa akichuana nae Bwana Siosi Sumari wa Chama cha Mapinduzi.
Kwamatokeo hayo yanafanya idadi ya Kura zilizompa ushindi Nassari wa Chadema kuwa kura 6,215 dhidi ya Sioi Sumari CCM.
Aidha Kagenzi ametangaza matokeo ya wagombea wengine ambao walishiriki uchaguzi huo kupitia vyama vyao vya Siasa nchini ambapo AFP wamepata kura– 139, DP -77, NRA – 35, SAU – 22, UPDB – 18 na TLP – 18.
Blog hii inampongeza Mh. Joshua Nassari kwa ushindi Mkubwa.
Blog hii inampongeza Mh. Joshua Nassari kwa ushindi Mkubwa.