RACHEL SCHARP AU MAARUFU KWA JINA LA RACHEL MASHAURI SCHARP NDIYE MWIMBAJI WA KITANZANIA ANAYEFANYA VIZURI SANA KATIKA HUDUMA YA UIMBAJI NJE YA NCHI HASA KATIKA NCHI ZA SWEDEN NA NORWAY
Huyu ndiye Rachel Mashauri Scharp
Mimi ni mzaliwa wa kwanza kwenye familia ya watoto wanne. Nimezaliwa na kukulia DAR.
Kuimba nimeanza Nikiwa mdogo na kuandika nyimbo pia. Lakini sikuwa na wa kuniendeleza. Nilikuwa naandika nyimbo nawafundisha wadogo zangu jioni tukisubiri ubwabwa Tunaimba. Nikiwa secondary nilikuwa nikiimba kwenye kwaya ya shule
Niliimba na kuongoza sifa Pia kwenye
fellowship ndogo huko Msewe. Pale ndipo nilipoona Naitwa kuimba. Nilipomaliza sekondari na kuingia chuoni sikuimba lakini kama ikitokea wakati nikiimba watu waliniambia aisee kumbe una Sauti nzuri Hebu jiendeleze. Lakini Mimi sikuwa na uwezo kwani nimetokea kwenye familia maskini
Mtu Wa kwanza ambaye aligundua kipaji changu ni marehemu Kaisy baba yake Nnunu Nkone mke pastor Donis Nkone. Mimi nilikuwa mtu Wa aibu sana nilikuwa natamani Sana kuimba na Marafiki zangu wengi walikuwa waimbaji kama Upendo Kilahiro, Nnunu Nkone, Daniel Kyara. Hawa walikuwa na kikundi chao, nilikuwa natamani lakini nashindwa kusema naomba kuingia. Lakini kila wakifanya matamasha au wanakwenda kuimba sehemu fulani Mimi Sikosi nawatamania. Na wala sikuwahi hata siku moja kuimba mbele yao nilikuwa naogopa. Ila baba yake Nnunu Ndio niliweza kuimba na nikamwambia Nina nyimbo Nataka kutengeneza album akaniambia atanisaidia kunifundisha, lakini sikufikia malengo hayo akafariki.
Rachel akiwa na wanae Henning na Makenga
Mimi Pia ni mwanamichezo Wa miaka mingi Sana kwenye level ya juu kidogo
Rachel akiwa na Mr wake Mr Martin Scharp
Nikiwa nasoma nilijishughulisha Pia na michezo tena Sana, nilicheza netboll, nimekimbia riadha mita 100 na mita 1500,nilicheza basketball timu ya vijana girls,netboll nilisajiliwa na timu ya magereza Tabora daraja la pili, polisi Arusha nimefanya nao mazoezi,st. James na excutive 11 .mpira wa miguu timu executive 11 n st.James Arusha, tulikuwa Kama waanzilishi as Mpira wa miguu kwa wana wake mkoani Arusha.
Mwaka 2002 nilichaguliwa na timu yangu ya St. James Kwenda nchini Norway kuiwakilisha.
Mwaka 2002 nilichaguliwa na timu yangu ya St. James Kwenda nchini Norway kuiwakilisha.
Nilivyohamia huku nikasimama na kwaya ya Elim Pentecostal church
Rachel akiwa na marafiki zake
Ni kwamba chochote unachokililia Mungu anasikia na atajibu kwa Wakati wake. Hata Kama itapita miaka mingapi itakuwa tu kwani huo ndio unakuwa Wakati aw Mungu, wala usihuzunike. Mungu anaaangalia nia ya ndani. Ni kumuimbia Mungu katika roho na kweli
Rachel akiwa location kwaajili ya video
Hapa Rachel akiimba pamoja na Shalom music International Choir
Rachel akihudumu
Albamu ya kwanza ilijulikana kwa jina la NARINGA NA YESU na hii ya pili inajulikana kwa jina MUNGU WA AJABU
Rafiki bado nakuombea Mungu akubariki
PAMOJA kwa UMOJA