KARIBU

KARIBU UPATE HABARI MBALIMBALI KUPITIA BLOG HII;;pamojakwaumoja2012.blogspot.com.
AU PIGA simu 0715408566 kwa Ushauri na maoni

KAULI MBIU/SLGN


HOPES

Monday, July 30, 2012

GAFLA BAHATI BUKUKU AANZA KUFANYA VYEMA BAADA YA KUTOA NYIMBO MPYA

BAHATI BUKUKU AMETEKA HISIA ZA WASIKILIZAJI WENGI HASA ZA WANAWAKE  BAADA YA KUTOA NYIMBO MPYA IJULIKANAYO DUNIA HAINA HURUMA.
Bahati Bukuku kama anavyoonekena katika picha
Jana nilifanikiwa kuzungumza naye kwa njia ya simu na mazungumzo yalikuwa hivi

Hellow mtumishi wa Mungu bwana yesu asifiwe?
Amen" habari ya uzima kaka yangu?
Nzuri sana dada yangu habari za wapi tena mtumishi
Dah! nipo tu kaka yangu kwani vipi sipatikani hewani? eeti hellow??
Hapana sio kwamba haupatikani hewani naona hatuonani kama awali tulivyokuwa tunapishana mtaani
Hapana kaka yangu niko mkoani Kilimanjaro ndiyo maana hatuonani.
Okey ndiyo maana sikuoni nilikuwa nadhani uko location kwa ajili ya Filamu.
Hapana!! ishu ya filamu bado ila bado nina pokea maombi ya watu wanaotaka kuwa katika filamu hii
Okey!!Aiseee Kilimanjaro nasi Mwanza ambako ulikuwa wiki iliyopita?
Kaka yangu we acha tu!! niko Kilimanjaro tena ndani ndani huku! Mungu anasaidia huduma inawafikia watu.
Dah!! umeongea kuhusu Moshi umenikumbusha maeneo ya Bomang'ombe.
Hahahahahahaha!!! nilipita juzi nikitokea maeneo ya Sanya juu!.
Hahahahaha!! dah! si utani kazi ya bwana inasonga mbele.
Okey tuachane na hayo niambie unajisikiaje watu walivyoipokea kazi yako mpya 
Hakika nazidi kumshang'aa sana huyu 
Mungu jinsi ambavyo anazidi kunitendea juu ya kazi hii mpya tayari huwezi kuamini kaka yangu  nimeshaitwa sehemu nyingi sana  nimebaki najiuliza wameisika wapi wakati ina muda mchache hewani.
Dada acha Mungu aitwe Mungu kwani yeye ndiye muweza wa yote maadam umemuimbia yeye hili ndilo jibu watu wanapata kuhudumiwa kupitia nyimbo zako so Mungu hawezi kaaa kimya juu ya ujumbe wake kuwafikia watu wake.
Ni kweli kaka yangu nakubaliana na wewe kwa usemi huo!
Jana nilikuwa nazungumza na mmoja kati ya msikilizaji wa redio aliniambia umemgusa maisha yake na tena anaomba kama itawezekana iigize katika filamu hii kwa maan ani maisha yake halisi yaliyo katika wimbo wako.!
Weweee! kweli anasema kila kitu nilichokiimba humo ndiyo maisha yake halisi
Yeah!! asilimia kubwa ni sehemu ya maisha yake halisi.
Mtumishi ya kuongea yako mengii la ngoja nikuache na mimi niendelee na maandalizi ya kipindi cha usiku(Kesha na PPR).
Okey kaka kila lakheri tutaonana kati ya jumatatu nikitoka Moshi,pia na mimi ngoja nijiandae maana napanda jukwaani muda si mrefu.
Ok barikiwa sana pia huduma njema!
Haya kaka yangu mungu akubariki sana wewe na watangazaji wenzako wote hapo!sorry nasiki kama nyimbo yangu hewani??
Yeah!! hahahaha! iko hewani siunajua watu wameipenda.
bye byeeeee!!!! 
Haya ndiyo yalikuwa mazungumzo kati yangu na Dada Bahati Bukuku akiwa Kilimanjaro(Moshi).

Rafiki bado nakuombea Mungu akubariki
Pamoja kwa Umoja

GARI LATUMBUKIA BAHARI

SIKU YA LEO MAJIRA YA ASUBUHI GARI LATUMBUKIA BAHARINI LIKIWAHI KUINGIA KWENYE BOTI(FELI)PANTONI
Dereva wa gali hilo aliruka na kutoweka kusikojulikana ila bahati nzuri wavuvi walishirikiana na kufanikiwa kuliopoa gari hilo
Ferry likiwa limebeba abiria kuelekea kigamboni

Angalia jinsi ambavyo ferry linavyobeba abiria na mizigo,pia angalia jinsi gani hatari hasa vyombo kama magari amabvyo yanaweza zama.

Tazama jinsi amabvyo gari limezama baharini.

Tazama abiria ambavyo huwahi kushuka katika pantoni kabla halijasimama

Tazama hapa jinsi ambavyo meli au boat ilivyozama bahari Hindi,Swali langu kwa wahusika wa usafirishaji baharini kwamba matukio haya yana maanisha nini au nini kinasababisha haya yote kutokea.Samahani ninaanza kuamini ipo siku pantoni litazama japo naiuwa hakuna anyependa kusikia maneno haya.ipo siku na si mbali

Rafiki bado ninakuombea Mungu akubariki
Pamoja kwa Umoja


GAZETI MWANAHALISI LAFUNGIWA

GAZETI MWANAHALISI LAFUNGIWA NA SELIKARI

Kubenea ambaye ndiye mmiliki wa gazeti mwanahalisi



Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imelifungia kutochapishwa gazeti la MwanaHalisi kuanzia 30 Julai, 2012 kwa muda usiojulikana kutokana na mwenendo wake wa kuandika habari na makala za uchochezi, uhasama na uzushi likiwa na nia ya kusababisha wananchi kukosa imani na vyombo vya dola hali inayoweza kuhatarisha amani na mshikamano uliopo nchini.

Katika matoleo yake hivi karibuni, gazeti la MwanaHalisi toleo Na. 302 la Jumatano Julai, 11 – 18, 2012 na toleo Na. 303 la Jumatano Julai 18 – 24, 2012 na toleo Na. 304 la Jumatano Julai 25 hadi 01 Agosti, 2012 na mengine yaliyotangulia yamekuwa yakichapisha habari na makala zenye kueneza na kujenga hofu kwa jamii.

Mhariri wa gazeti la MwanaHalisi, ameitwa na kuonywa mara nyingi, lakini hataki kukiri kuwa maudhui ya makala zake hazina tija kwa jamii, pia hazifuati weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari.

Mhariri, mara zote katika utetezi wake amekuwa akinukuu kifungu cha 18 cha Katiba ya nchi yetu ambacho kinatoa uhuru wa kutoa maoni na kwa makusudi kutonukuu kifungu cha 30 cha Katiba hiyo kinachoweka ukomo wa uhuru.

Uamuzi wa Serikali

Serikali imeamua kulifungia kutochapishwa kwa muda usiojulikana gazeti la MwanaHalisi, kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976, kifungu Na. (25) (i), adhabu hiyo itaanza tarehe 30 Julai, 2012 kwa mujibu wa Tangazo la Serikali (Government Notice) Na. 258 lililochapishwa katika Gazeti la Serikali na kutolewa jijini Dar Es Salaam tarehe 27 Julai, 2012.

Serikali inawataka wamiliki, wahariri na wanahabari kuzingatia sheria, uzalendo, weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari katika kutekeleza wajibu wa kuhabarisha, kuelimisha na kutoa burudani kwa wananchi.

Kama ilivyoelezwa Bungeni wakati wa kuwasilisha Bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo hivi karibuni waandishi na watangazaji wa habari wanatakiwa kuhakikisha kuwa habari wanazoziandika na vipindi wanavyoandaa vinazingatia taaluma na kuweka mbele maslahi ya Taifa letu na uzalendo. Uhuru na haki ya vyombo vya habari uendane na wajibu.

Kuanzia sasa Serikali haitasita kuchukua hatua dhidi ya vyombo vya habari ambavyo kwa maksudi vitatoa taarifa za uchochezi ambazo zitahatarisha hali ya amani na utulivu uliopo nchini mwetu.

Imetolewa na

OFISI YA MSAJILI WA MAGAZETI
WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
30 Julai, 2012

Ok waweza kuimba wimbo wa Tanzaniaa Tanzania Tanzania
Rafiki bado nakuombea Mungu akubariki
Pamoja kwa Umoja

DEBORAH SAID AZINDUA VIDEO YA ALBAM YA MTI WENYE MATUNDA.

VIDEO YA MTI WENYE MATUNDA YA MTUMISHI WA MUNGU DEBORAH SAID YA ZINDULIWA NDANI YAKANISA LA MAISHA YA USHINDI AMBAKO NDIKO MTUMISHI HUYU ANAHUDUMU,CHINI YA MUMEWE MCHUNGAJI JOHN SAID::
Hili ndilo kanisa la maisha ya ushindi ambako uzinduzi umefanyika wa mti wenye matunda wa Deborah Said.

Hili lilikuwa ni tukio la mgeni mtumishi wa Mungu Thomas Mwakalibule kuzindua audio cd akiwa na mtumishi wa Mungu Deborah Said mwimbaji/mama mchungaji

Mgeni akikagua ni jinsi gani teknolojia ilivyotumika katika kuitengeneza Cd hii,tunaona wakicheka kidogo sambamba na Mc wa shughuli hii Douglass Pius mtanagazaji wa redio ya dini Praise Power

Bado mgeni akizitazama kwa makini Cd hizi zenye albamu ya MTI WENYE MATUNDA

Mc wa shughuli hii mtumishi wa Mungu mwimbaji Sifa John akitoa maelekezo fulani katika uzinduzi huu.

Mc wa shughuli hii mtumishin wa Mungu Douglass Pius akimkaribisha mgeni katika madhabahu ya bwana.

Mtumishi wa Mungu mwenyeji mchungaji John Said akiwa na mgeni wake mchungaji Michael Anaki toka huduma yaAkuzamu


Mchungaji Michael Anaki toka huduma ya Akuzamu akizindua Video Cd ya mti wenye matunda.


Tayari kwa ishara hii Video Cd ya mti wenye matunda imezinduliwa rasmi na mchungaji Michael Anaki.

Mtumishi wa Mungu toka huduma hii chini ya mchungaji John Said akitoa neno juu ya utoaji katika shamaba la bwana,anasema unapotoa au kushiriki jambo lolote lenye kumpa Mungu Utukufu basi unakuwa umemkopesha Mungu so hivyo kwako wewe ambaye uko mahali hapa na yeyote yule atakayeona kazi hii kwa njia ya Tv basi anayo nafasi ya kushiriki baraka za bwana kwa kununua kazi hii ya mtumishi wa Mungu Deborah Said albamu ya MTI WENYE MATUNDA.

 KATIKA ENEO LA SIFA alikuwepo Norbert producer kutoka YEHOVA studio inayopatikana makongo juu.



Pia Chris na madam Ruth walikuwepo wakihuduma mahali hapa


Kutoka Kigoma mpaka Dar es salaam kama ambavyo yeye hupenda kusema mara kwa mara anaitwa mtumishi wa Mungu Victor Aron mwimbaji na mtanagzaji toka Praise Power Redio 99.2fm.Ambaye naye albamu yake iko njiani na tena muda si mrefu itakuwa hewani/madukani.

Dhumuni la uzinduzi huu lilikuwa ni kuchangia ujenzi wa kanisa la Maisha ya ushindi linalopatikana Ubungo Extenal na ndiko anakopatikana mtumishi wa Mungu Deborah Said ambaye ni mke wa mchungaji John Said.Milango iko wazi kwa ko wewe ambaye utasikia wito ndani ya moyo ukisema na wewe juu ya kushiri baraka za bwana katika kumtolea yeye katika ujenzi wa kanisa(hema la bwana) au nyumba ya ibada.
Waimbaji wengi walikuwepo ikiwa ni pamoja na Tina Malego,Neema Jekonia na wengine wengi,pia watu walikuwe ni wengi sana tofauti na ambavyo walitegemea wengi.

Rafiki bado nakuombea Mungu akubariki
Pamoja kwa Umoja

ABEDDY NGOSSO/SARA K

FANUEL SEDEKIA NA UPENDO WA YESU-MUNGU AKUBARIKI