KARIBU

KARIBU UPATE HABARI MBALIMBALI KUPITIA BLOG HII;;pamojakwaumoja2012.blogspot.com.
AU PIGA simu 0715408566 kwa Ushauri na maoni

KAULI MBIU/SLGN


HOPES

Wednesday, August 15, 2012

JE WAMJUA(WAMFAHAMU) PAUL MWANGOSI


ROHO MTAKATIFU,EBENEZA,NASIKIA KUITWA NA NYIMBO NYINGINE NYINGI NDIZO ZINAZOJULIKANA NA WENGI ZIKIWA ZIMETUNGWA NA KUIBWA NA MTUMISHI WA MUNGU PAUL MWANGOSI BABA WA MKE MMOJA NA MTOTO MMOJA
Mtumishi wa Mungu Paul Mwangosi katika picha

(Mke)Mrs paul Mwangosi

Binti wa Paul Mwangosi

Paul Mwangosi
 Hawa ni vijana wa kazi Wayahudi halisi hawana mchezo na maagizo ya Mungu wao wanasikiliza sauti moja tu kutoka kwa Mungu hiyo ni sheria ya Israeli majadiliano baadaye kazi kwanza

Paul Mwangosi Hapa ndiyo Golgota kama unavyosikia fuvu la kichwa juu ya kilima hiki ndipo Yesu aliteswa ni nje ya Yerusalem ya zamani AMEN

Paul Mwangosi Mahali hapa ndipo Yona alipanda Merikebu ili amkimbie Mungu na alitapikwa kando kando hii ni Israel
Paul Mwangosi Mtumikie Mungu kwa moyo wako wote uwe sadaka ninakumbuka utumishi wa ndugu huyu unyenyekevu wake nilichojifunza alikuwa ni rafiki wa Yesu, Je wewe una chapa za kristo tunaweza kupata matunda kwako ?

Paul Mwangosi akiwa na marehemu Fanuel Sedekia katika huduma ya bwana.
WARUMI 12;1-2 ,Basi ndugu zangu nawasihi kwa huruma zake Mungu itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai takatifu ya kumpendeza Mungu ndiyo ibada yenu yenye maana,2 Wala msiifutishe namna ya dunia hii,bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu,mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema ya kumpendeza, na ukamilifu

PAUL MWANGOSI
Mtumishi huyu Paul Mwangosi anapatikana katika kanisa la Azania front,pia amekuwa akipatikana na kuonekana katika semina za mwalimu Christopher Mwakasege,amekuwa akiongoza sifa na kuabudu.Mwimbaji huyu amefanikiwa kurekodi albamu aliyoipa Jina la Tunapanda Yerusalem,ambapo kuna nyimbo kama
BABA YETU,HALELUYA,HOSANA,IKISA IKI,JINA L AYESU,KIMBILIA KWA YESU,NAKUHITAJI YESU BWANA,TUNAPANDA YERUSALEM NA TWAOMBATUTAKIANE AMANI.
Baada ya kutoa nyimbo alikaa kimya kidogo kisha akaja kutoa nyimbo nyingine ambazo pia ndani yake alimshirikisha mke wake mpenzi,kitu cha ajabu katika familia nilichokiona kwa mtumishi huyu ni uimbaji kuanzia babu yake baba yake mama yake kisha yeye na mkewe na  mtoto wake,mtoto anakaribia kukamilisha albam yake vile vile yeye mwenyewe Paul yuko katika harakati kutoa nyimbo nyingine baada ya kumaliza safari za huduma ikiwa ni safari za kuzuru Izrael na semina mbalimbali za hapa ndani ya nchi.
Nilifanikiwa kuongea na mama yake mzazi Paul Mwangosi yeye kwa maelezo yake anasema alimpokea(aliokoka) bwana yesu mwaka 1966 katika mazingira ya taabu kutokana na jamii kumshangaa nini alichokifanya,anasema katika miaka hiyo ya wokovu wao walikuwa wanaonekana kama ni watu wa ajabu walipotea  kabisa,ila haikumpa shida kwa maana alijua hiyo ilikuwa ni vita ya falme mbili katika ulimwengu wa roho na mengine mengi kama hayo.
Paul yuko kwenye harakati za kukamilisha kitabu chake kitakachokuwa kikifundisha jamii katika mambo  tofauti tofauti hasa ya uimbaji kwa kuwa yeye pi ni mwalimu wa kusifu na kuabudu.
Paul Mwangosi anampango wa kuandaa tamasha la kumsifu Mungu na kuabudu katika roho na kweli,so muda si mrefu mambo yote yatajulikana(yatakuwa open)na yatatangazwa kupitia vyombo vya habari.

Behind the scene Paul Mwangosi ni mtaalamu sana wa mambo ya Video Production na yuko na mambo fulani anayaweka sawa ili wakati ukifika afanye vitu vikubwa katika mambo ya video.Kwa niaba yangu na wana Blog tunakutakia kila lakheri na uzima na afya njema ili kuyafikisha mbali hayo maono.

Rafiki bado nakuombea Mungu akubariki
PAMOJA kwa UMOJA.

ABEDDY NGOSSO/SARA K

FANUEL SEDEKIA NA UPENDO WA YESU-MUNGU AKUBARIKI