KATIKA MAISHA YA BINADAMU YAKO NA PANDE MBILI TOFAUTI AMBAZO NI KUPANDA NA KUSHUKA NDIYO MAANA KUNA USEMI USEMAO HUJAFA HUJAUMBIKA.JIFUNZE KUPITIA SEHEMU HII.
WAHENGA walisema hujafa hujaumbika na hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Emmanuel Mwakisunga Jumamosi Juni13, 2004 alipopata pigo ambalo lilibadili kabisa mtazamo na mwelekeo wa maisha yake. Ajali mbaya ya gari ilisababisha apate jeraha kubwa shingoni, utumbo ukatoka nje, mguu wa kulia na mkono wa kulia vikavunjka mara tatu. Akiwa bado kijana mdogo mwenye miaka 22 tu, ndoto zake nyingi zimeyeyuka kama barafu ndani ya moto mkali.
Hakutarajia hayo lakini hali ndivyo ilivyo, hivi sasa amepata ulemavu wa maisha.
“Kwanza mimi kupona ni Mungu pekee, kwa sababu katika ajali ile nilinusurika mimi peke yangu wengine wote walikufa. Ilikuwa ni ajali mbaya sana, ambayo imenifanya niwe hivi unavyoniona.” “Nimezaliwa Mbeya mwaka 1988, wazazi wangu wote ni wenyeji wa huko, tulizaliwa watoto tisa mimi nikiwa wa tano. Baba yangu ni mtumishi wa Mungu na mama yangu anafanya kazi za ndani kwa mtu,” anadokeza kidogo kuhusu familia yao.
“Kwanza mimi kupona ni Mungu pekee, kwa sababu katika ajali ile nilinusurika mimi peke yangu wengine wote walikufa. Ilikuwa ni ajali mbaya sana, ambayo imenifanya niwe hivi unavyoniona.” “Nimezaliwa Mbeya mwaka 1988, wazazi wangu wote ni wenyeji wa huko, tulizaliwa watoto tisa mimi nikiwa wa tano. Baba yangu ni mtumishi wa Mungu na mama yangu anafanya kazi za ndani kwa mtu,” anadokeza kidogo kuhusu familia yao.
Emmanuel alikomea darasa la sita baada ya kukosa karo ya shule alipata kazi ya utingo katika magari yatokayo Dodoma kwenda Morogoro. “Mwaka 2002 nilianza kazi hiyo ya utingo. Nashukuru kwamba ilikuwa ikinipatia senti mbili tatu ambazo zilinisaidia kula na kuvaa kwa sababu wazazi wangu hawakuwa wakijiweza kifedha,” anasema Emmanuel. Maisha yake yalibadilika akiwa na umri wa miaka 16 tu.
Siku hiyo basi lilikuwa limejaa pomoni na yeye akiwa utingo alikuwa amesimama mlangoni akihudumia abiria. “Tulijaza abiria siku hiyo hata nafasi haikutosha, mimi nilikuwa nimesimama mlangoni kama kawaida ya utingo. Tulikuwa tunatokea Dodoma tukielekea Morogoro majira ya saa kumi jioni. Gari letu lilikuwa linafukuzana na Fuso ambalo lilikuwa linataka kutupita.
Kusema kweli hakukuwa na sababu ya dereva wetu kukimbizana na Fuso lile, basi tu ilikuwa ni ujana na ujinga,” anasema Emmanuel na kuongeza: “Gari letu likiwa katika mwendo mkali kupita kiasi ghafla mbele yetu tukaona lori aina ya Scania kubwa la mizigo likiwa linaelekea pia Morogoro, kwa kuwa gari letu lilikuwa katika mwendo mkali, lilishindwa kufunga breki, kwa hiyo likaingia nyuma ya scania hilo.
Wakati tukio hilo linatokea mimi nilikuwa nashuhudia kila kitu, nikataka kurudi nyuma ili niepuke kuumia kwa kuwa nilikuwa mbele, lakini ilikuwa ni vigumu kwa sababu gari lilikuwa limeshona.” Alisikia mlio mkubwa na sauti za vioo vikivunjika kisha likabinuka na kusererekea upande wa kushoto. Kutokana na kasi ile, alitupwa nje na bati moja lililotoka katika basi lao lilimwingia tumboni. “Nikarushwa nje hadi chini kwenye lami, bati likang’oka katika gari letu, likaniingia tumboni na kuzama kabisa nikawa najaribu kuling’oa lakini ikawa ni ngumu.
Mpaka sasa sielewi lilitokaje, nikajikuta pembeni na nikawa nashuhudia utumbo wangu ukiwa nje.” “Mpaka nafikishwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro nilikuwa najitambua, nikawapa madaktari namba za simu za baba. Sikuwa nasikia maumivu, nilipofika mlangoni mwa hospitali tu, fahamu zikanipotea. Kwa mbali nikamsikia muuguzi akisema muwekeeni damu haraka.” Fahamu zilimrudia baada ya siku moja, wazazi wake walifika na kumkuta akiwa hoi, walimhamisha na kumpeleka Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
“Tulipofika Dodoma madaktari wa pale walisema nimecheleweshwa sana, hivyo mkono na mguu vimeshaharibika na endapo wataviacha hivyo, basi uwezekano wa sumu kusambaa hadi kwenye moyo ni mkubwa na ungesababisha kifo changu. Baba na mama wakaulizwa kama wamekubali nikatwe mkono na mguu,
Hawakuwa na la zaidi isipokuwa kukubali ili angalau wanione nikiwa hai.” Pamoja na wazazi wake kukubali, lakini bosi wake, mmiliki wa gari lililopata ajali, anayemtaja kwa jina la Mzee Kindole, hakutaka kusikia Emmanuel anakatwa mguu wala mkono, aliwaomba madaktari wajaribu njia nyingine za matibabu ili kijana huyo apone akiahidi kutoa gharama zote kwa kazi hiyo lakini haikuwezekana.
“Siku ambayo sitaisahau ni tarehe 20 mwezi wa sita, 2004, nilishtuka alfajiri nikawa nataka kwenda haja ndogo, nikajaribu kushusha mguu chini ili nitembee ukawa haushuki. Nikataka kushika mguu huo kwa mkono nao ukawa haufanyi kazi. “Baba yangu alikuwa pembeni yangu akaniambia: 'Usijali haya ndiyo maisha ambayo Mungu amependa uishi cha muhimu ni kuwa bado ungali hai.'
Akaendelea kuniambia 'mwanangu Emma umekatwa mguu na mkono wa kulia.' Nililia sana sikuamini, nikatamani kufa lakini baba yangu alinitia moyo kwa kiasi kikubwa namshukuru sana.” Alikaa hospitali kwa miezi minne na alipopata nafuu aliruhusiwa, lakini kulingana na hali ya maisha ya familia yake, ilimbidi apigane na maisha, atafute mkate wake wa kila siku.
Akaingia mtaani na kuanza kupiga debe kwenye daladala na ndipo alipwe ujira. Alikuwa akipata Sh200 au 100 kwa kila gari. “Wakati mwingine naomba barabarani lakini napenda zaidi kupiga debe kwa sababu kabla sijapata kilema nilikuwa nafanya kazi kwenye magari halafu sipendi sana kuomba watu fedha,” anasema. Emmanuel ni tofauti na walemavu wengi, anatamani afanye biashara kwa sababu hapendezewi na hali ya kuombaomba na kupiga debe. Kinachokwamisha yote hayo ni mtaji kwani pamoja na kubaki na mguu na mkono mmoja anasema anaweza kuuza nguo za kike na za watoto. Anapatikana kwa namba.
Mpaka hapa ninamatumaini kwamaba utakuwa umejifunza kitu toka kwa Emmanuel
Mpaka hapa ninamatumaini kwamaba utakuwa umejifunza kitu toka kwa Emmanuel
Rafiki bado nakuombea Mungu akubariki
PAMOJA kwa UMOJA