KARIBU

KARIBU UPATE HABARI MBALIMBALI KUPITIA BLOG HII;;pamojakwaumoja2012.blogspot.com.
AU PIGA simu 0715408566 kwa Ushauri na maoni

KAULI MBIU/SLGN


HOPES

Sunday, July 15, 2012

MFAHAMU MTUMISHI WA MUNGU (MWIMBAJI) HANS AZZAD


KATIKA KUKUONYESHA NINI MUNGU KAWEKA NDANI YAKE:


Mtumishi wa Mungu Hans Azzad katika pozi
Katika maisha nimejifunza mambo mengi sana na nimejita nakuwa watofauti kila siku ki fikra na hata  kimaamuzi,hii ina maanisha nini tuwe ni watu wa kujifunza kila  siku bila kuchoka(kukoma) kwa maana elimu haina mwisho.Nimejisikia kuanza na maneno hayo kwa maana gani,katika maisha na life story ya mtumishi wa Mungu Hans Azzad nimejifunza sana kupitia yeye kwa maana amepita katika maisha ya vijana wengi ambao asilimia kubwa wanatamani sana maisha kama ambayo yeye ameyapitia.





Mnamo miaka kadhaa iliyopita alipata nafasi ya kusoma nje ya nchi(South Africa) baada ya kumaliza masomo yake nchini huko akaamua kuanza maisha rasmi huko nchini Africa ya kusini bila kujua ataishije na ataanza vipi maisha kwanza akamuamua kuingia kwenye biashara yakusafirisha madawa kulevya kwenda nchi za Ulaya na Amerika.

Mtumishi wa Mungu Hans Azzad
Alifanikwa fuifanya kazi au biashara hiyo kwa muda mrefu huku na uzoefu ukiongezeka,sasa akaanza kusafiri mwenyewe na kuanza kutafuta masoko yake mwenyewe,mara ya kwanza alikuwa akifanya biashara chini ya mtu mwingine yaani akiwa ameajiliwa,baada ya kuzoea akaanza kubeba mzigo wa kampuni huku akibeba na mzigo wake mwenyewe,soko lake lilikuwa hapo hapo nchini Afrika ya kusini na hakuwahi hata siku moja kuwaza kuleta hapa nyumbani.Katika biashara hiyo ya kusafirisha madawa ya kulevya alijikuta mara kwa mara akiingia matatani kwa kukamatwa na polisi na kufungwa katika magereza tofauti tofauti ya nchi tofauti ikiwa ni pamoja na Ulaya na nchi za Amerika ya kusini nchi za Brazil na Mexico.Baada ya kufanikiwa kutoka gerezani alifanikiwa kubeba tena mzigo toka nchi ya Hispania mpaka Afrika ya kusini,bila kujua ndani ya tumbo lake,aliko bebe mzigo huo kulikuwa kumeanza kuhalibika,kwa madawa yale kusababisha utumbo kuvimba na kutengeza kitu kama kibofu kilicho beba madawa hayo,hali ilikuwa mbaya kwake hadi kufikia hatua ya kutakiwa kufanyiwa operesheni.Baada ya kuambiwa anatakiwa kufanyiwa Operesheni alizungumza moyoni na kusema ni bora Mungu amchukue (anichukue) kuliko kubaki kuishi tena,hii ni kutoka na yeye kujiona kama ni mtu asiyefaa tena kuishi kwa mtizamo wa kibinadamu bila kujua kuwa Mungu anamtafuta kuja kuwa mtumishi wake.Operesheni ikafanyika kwa utalaamu wa hali ya juu sana na kwa tahadhari kubwa,hatimaye  zoezi la upasuaji likakamilika,Hans akiwa katika usingizi mzito gafla akazinduka usingizini alijikuta yuko sehemu asiyoijua ikiwa imejaa mtambo ya hali ya juu na akipumlia mashine ndipo daktari alitokea na kumwambia uko hapa kwaajili ya matibabu na umefanyiwa upasuaji na haikuwa lahisi bali ni Mungu tu amefanya maajabu kwa maana utumbo ulikuwa umeharibika sana.Baada ya hayo yote gafla Hans akaisikia sauti ya Mungu ikizungumza naye kuwa sasa yeye ni mtumishi wa Mungu,Hans akajiuliza inakuwaje mimi leo niwe mtumishi wa Mungu angali nilikuwa nafanya mambo yasiyofaa kabisa katika jamii yote,na hapo kabla alikuwa ni mtu anaye washangaa sana watu waliokuwa wanakwenda kanisa na kwenye mikutano ya Injili.Sauti ya Mungu haikuishia hapo ikawa bado kila wakati inasema naye kwa mazingira ya tofauti tofauti na moja kati ya maneno ambayo alikuwa anayasikia yakisema naye ilikuwa inasikika ikisema wewe ni mwanangu wathamani sana tena nakuwazia mawazo yaliyo mema na sasa nahitaji unitumikie,hapo ndipo akagundua kuwa kumbe bado yeye ni wathamani mbele ya Mungu.Taratiibu akaanza sasa kusoma biblia nakuona maneno mengi yenye kumfariji sana na yenye kumtia moyo juu ya kumtumikia Mungu,mwanzoni alikuwa akijiuliza ana nini chenye kumpa Mungu utukufu,lakini ndani ya biblia akakutana na maandiko ya mazuri yanayo mzungumzia Mfalme Daudi alivyoupata ufalme bila kujali mkononi alikuwa ana nini na kumpiga Goliati.Hans alirudi nyumbani Tanzania toka nchini Afrika yakusini baada ya keshi yake juu ya biashara hiyo aliyokuwa akiifanya huko,kesi yake ilimgharimu zaidi ya Tsh milioni 300.Hivi sasa Hans ni mwimbaji wa nyimbo za injili na amefanikwa kukamilisha albamu yake aliyoipa jina Asante Yesu.Tamani sana kukutana nae ili akupe ushuhuda wake katika safari yake ya ujana na maisha.Moja kati ya nyimbo ambayo inapatikana katika albamu yake na imetokea kupendwa na wasikilizaji wengi wa redio za kiinjili ni nyimbo YOUR SO CLOSE TO ME,nyimbo inafanya vizuri sana iko katika mahadhi ya reggae,hakudhani kama ipo siku atakuja kumwimbia na kumtumikia Mungu kama ilivyo sasa tena kwa kiwango kikubwa.Yako mengi sana yanayomhusu Hans ila mpaka hapa najihisi kama nimekufikisha sehemu fulani ya kumtambua Hans japo kwa sehemu.Nikutakie amani ya bwana katika safari yako ya maisha ya kila siku ila tambua kuwa Mungu ANAKUPENDA SANA.
Rafiki yangu badi nakuombea,Mungu akubariki
Pamoja kwa umoja

MTUME NA NABII JOSEPHAT MWINGIRA (EFATHA)

ABEDDY NGOSSO/SARA K

FANUEL SEDEKIA NA UPENDO WA YESU-MUNGU AKUBARIKI