KANUNI ZA KUIFIKIA FURAHA YA KWELI
Wakati
wa kutafuta furaha ya kweli lazima kujiuliza baadhi ya kanuni za kimaisha kama
unazifuata kwa ufasaha, vinginevyo unaweza kuwa mtafuta furaha lakini usiwe
miongoni mwa wanaoipata. Kama nilivyosema awali kuwa, kuna watu hutafuta furaha
kupitia kwa wake/waume zao, rafiki, wapenzi na hata kwenye mali, lakini mwisho
wa siku wanapokuja kutafakari zaidi hujikuta hawana furaha waliyoitaraji wakati
wakihangaikia njia za kuipata.
Kuna
watu ambao mawazo yao yanatamani sana kupata mtoto na wengine wameapa kabisa
kwamba wakifanikiwa kushika ujauzito watakuwa na furaha, lakini bado kama
hawatakuwa makini wao wenyewe watajikuta wanapata furaha ya muda na hatimaye
kutoweka na kuanza kujutia harakati zao, huku wakianza safari mpya za kufuata
furaha kupitia jambo jingine. Hebu tujiulize maswali haya.
A-Je
tunapokuwa tunatafuta furaha tunatumia uwezo wetu wote au kwa kiwango kidogo?
Kama tunatumia kiwango kidogo basi tujue kuwa hata kama tutapata kitu
tunachodhani kitatufurahisha utajikuta hatufurahi, kwa sababu hatutafanikiwa au
tutakuwa na furaha ya muda tu kwa vile nia yetu hatukuijaza kikamilifu ili
tuweze kupata furaha timilifu
B-
Je tunafanya sawa katika maamuzi au tunabahatisha tu? Endapo tutakuwa tunafanya
mambo ya kubahatisha ambayo hatujayahakiki, huzuni yetu itakuwa kwenye makosa
na kamwe hatuwezi kufanikiwa kupata yale tunayotaraji yatufurahishe. Kuna watu
wanatafuta watoto lakini hawazingatii kalenda za mimba na wengine wanatafuta
mali, elimu kubwa, mke mwema, lakini hawako makini katika kufanya maamuzi kwa
usahihi. Ni vema tukathibitisha uchaguzi wa mambo ili tufanikiwe kupata
yatakayotufurahisha.
C-
Je tunatimiza wajibu wetu au tunadanganya? Wapo watu ambao walitamani kuoa ili
wapate furaha, lakini walipofanikiwa katika hilo hawakutimiza majukumu yao
wakajikuta wanageukwa na wake/waume zao na kujutia uamuzi wao. Msomaji wangu,
unapokuwa katika safari ya kutafuta furaha kupitia utajiri, elimu, uongozi ni
vema ukatimiza wajibu wako, ili upate matokeo mazuri. Maana kama utakuwa
unatamani kufaulu mtihani wako halafu husomi kwa bidii, sina shaka majibu
utakayopata yatakuhuzunisha kwa sababu lazima ufeli na furaha uliyotaka
haitapatikana.
D-
Je tunafuata muongozo, au tunakiuka? Kila jambo tunalotaka kulifanya lina
kanuni zake, ukitaka kupika ugali upo muongozo ambao unakutaka uwe na vifaa,
uache maji yachemke na hata kutoharakisha upishi wenyewe, lengo ni kupata
matoke mazuri. Sasa kama tutakuwa kupata furaha ya kudumu kupitia mambo fulani
ni lazima tuyafanye kwa kufuata muongozi na si kwa kukurupuka. Biashara, elimu,
kazi, zote hizi zinamiongozo ambayo lazima kuifuata kwa matokeo mazuri.
E-
Tunatumia tulivyopata au tunavitelekeza? Wapo watu ambao hutamani kupata kazi,
lakini wanapopata hawazitumii, kazi hizo kwa ukamilifu, badala yake wanakuwa
watu wa kufanya ujanja ujanja ujanja kwa kutoroka na wakati mwingine
kutojihusisha na shughuli nyingine kwa lengo lile lile la kutafuta furaha.
Kusema kweli mtu wa namna hii hawezi kuwa na furaha kwa sababu anayolenga
yamfurahishe hayatumii kufurahika na badala yake anatafuta jambo jingine.
Fikiria kuhusu mume, anaoa lakini anaacha kumtumie mke wake wake anakwenda kwa
hawara! Hili si jambo jema na kamwe haliwezi kuleta furaha kupitia mambo
tunayoyatafua. Soma vifungu hivi ndani ya kitabu cha Biblia: “Vitu
vyote ni halila, bali si vitu vyote ifaavyo.
(1 Wakorintho 10:23).” “ Basi yeye
ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi (Yakobo
4:17)
”
Rafiki bado nakuombea Mungu akubariki
PAMOJA kwa UMOJA