KARIBU

KARIBU UPATE HABARI MBALIMBALI KUPITIA BLOG HII;;pamojakwaumoja2012.blogspot.com.
AU PIGA simu 0715408566 kwa Ushauri na maoni

KAULI MBIU/SLGN


HOPES

Thursday, August 23, 2012

WAINJILISTI SITA KANISA LA SCOAN KUTUA DAR

WAINJILISTI SITA WA KANISA LA SCOAN LA TB JOSHUA NCHINI NIGERIA KUTUA DAR ES SALAAM
Nabii TB Joshua
Wainjilisti sita kutoka kwa Nabii maarufu sana duniani TB Joshua wa kanisa la The Synagogue Church of all nation (SCOAN) la nchini Nigeria,wanawasili jumapili wiki hii.
Wainjilisti hao wanakuja nchini kwa  ajili ya shughuli maalum za kiinjilisti ambapo wataonana na waumini mbalimbali wa kanisa hilo,waliopo hapa nchini.
Nabii TB Joshua
Mratibu wa kanisa  hilo nchini ,Bi Martha Kaaya,alisema kanisa hilo lina makao makuu yake mjini Lagos Nigeria.
 
Wainjilisti hao watawasili Jumapili watakaa siku nne wakifanya kazi ya kuwasaili watu wanaotaka kwenda nchini Nigeria kwa maombezi.Watanzania 400 wameomba kwenda kupata huduma ya maombezi kwa Nabii TB Joshua kwa ajili ya maombezi na matatizo ya kiroho na kimwili.Wainjilisti hao wataonana na watu waliojiandikisha kwenda SCOAN,Nigeria kwa maombezi waje na ripoti za kitabibu na wawahi asubuhi ili kuwahi usaili,"alisema Martha.
Nabii TB Joshua
Agosti 28 na kesho yake wainjilisti hao wataonana pia na marafiki na wadau wa televition ya EMMANUEL saa mbili asubuhi katika ukumbi wa Diamond Jubilee na hivyo watu wote wawahi kufika ukumbini kabla ya saa mbili asubuhi.Kati ya watu 400 walioomba kwenda kwa Nabii TB Joshua,watakao shinda kwenye usaili huo ndiyo watakaoenda nchini Nigeria kwa mwaliko wa Nabii huyo.
 
 
Rafiki bado nakuombea Mungu akubariki
PAMOJA kwa UMOJA
 

MIEZI MIWILI YA MGUSO WA UPAKO BAADA YA UKIMYA MWINGI


MWIMBAJI BAHATI BUKUKU UFANYA KWELI KATIKA HEMA LA BWANA MLIMA WA MOTO
Bahati Bukuku katika madhabahu akimwimbia bwana
Bahati Bukuku
Bahati Bukuku
Waumini wa Mlima wa moto wakiongozwa na mchungaji Dr Getrude Rwakatare wakiendele kubalikiwa na nyimbo ya Bahati Bukuku "Dunia haina huruma"
 
Watu wakibarikiwa na wimbo Dunia haina huruma ya Bahati Bukuku

Baraka zikiendele kama picha ionyeshavyo




Nguvu ya Mungu ikifanya kazi madhabahuni
 
Bahati Bukuku anasema anataka kutengeneza na Mungu wewe Je??? unatengeneza lini?
 
Hakika kumbe ukimya wa muda mrefu ulikuwa na kishindo maana nyimbo hizi mpya za dada Bahati Bukuku zimeonekana kuwa bariki watu wengi,kama ilivyokuwa hata katika albamu zake za mwanzo.Barikiwa dada Bahati Bukuku Mungu awe nawe wakati wote umwitapo,barikiwa sana mdau wa injili na mpenda uimbaji  wakati wote MUNGU akutane na haja zako kila umwitapo.AMEN
Rafiki bado nakuombea Mungu akubariki
PAMOJA kwa UMOJA
 

ABEDDY NGOSSO/SARA K

FANUEL SEDEKIA NA UPENDO WA YESU-MUNGU AKUBARIKI