KUJERUHIWA AMA KUUGULIWA.
Watu
wengi wanapojeruhiwa hasa vibaya au kupatwa na magonjwa sugu yanayotajwa kuwa
hayana tiba hufadhaika sana. Mgonjwa kama kansa, kisukari, ukimwi, BP
yamewahuzunisha wengi, hii inatokana na hofu ya kufa, ingawa ukweli unabaki
kuwa kifo hakina ushirika na magonjwa hayo tu kwani kuna wanaokufa bila kuugua magonjwa
hayo.
Jambo
kubwa la kufanya ni kuondoa hofu kwa kuchukua mifano ya watu ambao
wameishi/wanaishi kwa muda mrefu wakiwa na magonjwa hayo, lakini hawajafa.
Usijifananishe na waliokufa mapema kwani inawezekana walikuwa na hofu ndiyo
maana wakafa. Hofu ndiyo inayotajwa kuua watu wengi kuliko hata magonjwa
yenyewe. Acha kufikiria mawazo ya kufa, usikate tamaa, endelea kufanya
mambo yako kama kawaida na uwe karibu na watu wa kukufariji si wa kukuvunja
moyo.
Usijihukumu
kuwa ni mkosa mbele ya jamii na usione kama umeonewa na Mungu. Tembelea
wagonjwa wengine hospitali, huko utaona wenye shida zaidi yako, hiyo itakupa
unafuu wa kubeba udhaifu wako. Kwa wale waliopata ajali ni vema wakakubaliana
na matokeo, wakatulia na kuwatembelea watu wenye ulemavu ili kupata msaada wa
kimawazo na wakati mwingine kufanya ibada ya kuomba wapewe uvumilivu.
Ifahamike
kuwa, ulimwenguni kuna walemavu wengi ambao wana maisha mazuri kuliko hata
wazima, hivyo basi kuwa kilema haimaanishi kuwa umefikia mwisho wa maisha.
NDUGU YANGU USILIE WALA KUKATA TAMAA MUNGU BADO ANAWEZA KUBADILISHA HISTORIA YAKO AMINI KUANZIA SASA KUWA INAWEZEKANA
Rafiki bado nakuombea Mungu akubariki
PAMOJA kwa UMOJA