HAKIKA KUSIFU NA KUABUDU PAMOJA UWEPO WA MUNGU HAUKAWII KUSHUKA.
The rivers team(John Lisu)
Glorious Celebration team
AIC
Team nzima ya kuabudu kwa vikundi vyote
Nimejifunza kitu katika kusifu na kuabudu pamoja na nimeona kuwa,kusifu na kuabudu pamoja inapendeza sana kuliko kila mtu anafanya vya kwake HONGERA sana kwa waandaaji wa mkesha uliofanyika katika ukumbi wa CCC Upanga.Penye uzuri hapakosi mabaya.Kwanza naomba nieleweke utaifa wangu kuwa mimi ni mtanzania halisi ninae jivunia kila kitu cha kitanzania,nilichokiona kizuri naomba nikiseme na nilichokiona si kizuri naomba vile vile nikiseme.Naomba kufahamu nini lengo la mikesha yetu yote tunayokuwa tunaiandaa maana yawezekana kimwonekano wa venue(mahali) tukafanikiwa lakini lengo letu tukafeli,kwanini nasema hivi kulikuwa na ulazima gani wa kutumia lugha mbili au kingereza kwenye kundi kubwa la watanzania au nini lengo au nani mlengwa wa mkesha,Samahani nasema hivi nikiwa na maana hii kwanini kitumike kiingereza wakati asilimia 95% ni watu wanao jua vizuri kabisa kiswahili,Kama mahubiri yanakuwa na mkalimani kwanini na nyimbo zisiwe na mkalimani kwa maana nyimbo ndiyo funguo za kukusogeza karibu na Mungu au ni utaratibu wa sehemu fulani kuabudu na kusifu kwa lugha ya kiingereza.Binafsi nilibarikiwa sana ila kuna maeneo ya msingi sana ya kuyafanyia kazi kama kweli lengo letu nikuwasogeza watu karibu na Mungu wao
Kitu kingine tittle(kichwa cha habari)kifanane na kile kinachofanyika pale sehemu husika kwa maana nimekuwa mmoja wa watu ambao nalazimika kuamini niko CLUB nasi ibaadani kama ambavyo kichwa cha habari cha mkesha,kwa mfano kichwa hiki cha habari A night of Worship kina maanisha ni usiku wa kuabudu sasa zinapoanza hip hop katika ya kuabudu tunakuwa tunaelekea wapi?? samahani huu ni mtizamo tu na nilazima tubadirike katika baadhi ya maeneo kama kweli tuna lengo lengwa(Target) hasa la kumtafuta Mungu,Sipendi kuamini kuwa haiwezekani kubadilika labda kama ndiyo utaratibu wa mahali husika,Swali langu kwanini kuna baadhi ya kumbi au makanisa kukiwa na mkesha asilimia kubwa ni vijana sioni wazee au watu wa makamo fulani je ni kwamba hawapati taarifa hizi za mikesha au kuna sababu za wao kutokuja katika mikesha hii au watu hawapati kile wanachotarajia kupata au hip hop zinawakimbiza wasije kuabudu.
Yote kwa yote nafurahia sana kuona watu wakimtafuta Mungu hata kuthubutu kuacha vitanda vyao,ila inasikitisha mtu kumkosa Mungu aliyemtegemea kumwona usiku ule badala yake anakutaana na vitu vingine kabisa.
OMBI LANGU KWA WOTE TUNAO ANDAA MIKESHA AU MATAMASHA::
>Ni lazima kujua nini lengo la mkesha au tamasha.
>Ni lazima kujua nani mlengwa wa mkesha au tamasha.
>Elimu haina mwisho na pia tujifunze kupokea mrejesho wa kile kilichofanyika toka kwa wadau(walio hudhulia)inasaidia kujua nini mapungufu au nini mafanikio.
Mwisho nashukuru wote wale ambao mmekuwa chanzo cha wengine kuwafanya wamrudie Mungu wao hakika Mungu atawalipa,ila tujitahidi sana kuondoa na kukemea roho ya USHAROBARO kwenye Gospel itawaangamiza vijana wenzetu ambao wanaifanya kazi ya Mungu kama kazi na mikogo mingi nasi huduma.
Bonyeza play ili usikilize wimbo huu hapa chini
Rafiki bado nakuombea Mungu akubariki
PAMOJA kwa UMOJA