KARIBU

KARIBU UPATE HABARI MBALIMBALI KUPITIA BLOG HII;;pamojakwaumoja2012.blogspot.com.
AU PIGA simu 0715408566 kwa Ushauri na maoni

KAULI MBIU/SLGN


HOPES

Friday, October 19, 2012

TANZANIA TANZANIA NAKUPENDA KWA MOYO WOTE

SISI SOTE NI WATOTO WA BABA MMOJA TUZIDI KUPENDANA NA KUIPENDA TANZANIA YETU NA KUILINDA
Bonyeza hapa imba wimbo huu

TANZANIA TANZANIA
TANZANIA TANZANIA
 
TANZANIA TANZANIA
TANZANIA TANZANIA
TANZANIA TANZANIA
Ndugu watanzania popote pale mlipo napenda! kuchukua fulsa hii kukumbusha mambo muhimu sana juu ya taifa letu hili,ya kwamba Uzuri na ubaya//AMANI NA UMOJA NA MSHIKAMANO viko ndani ya uwezo wetu,hatuna historia ya kubaguana wala kutengana kwa sababu ya Imani zetu,Pili tukumbuke hapa tulipofika sio sehemu ndogo ya kuchezea au kudharau umoja wetu wa siku zote,tumeishi miaka na miaka tukiombana mpaka chumvi na sukari pia kuombana miiko na masufuria je leo tunataka kupelekana wapi????
 
 Tukumbuke ya kuwa kokote duniani unakosikia kuna vita vya wenyewe kwa wenyewe vilianza hivi hivi na watu wachache hatimaye taifa zima likaingia vitani,Ombi langu kwa kila mtanzania tukumbuke kuwa kwanza Tunaishi kwa neema tu! ya Mungu,pia Mungu anamakusudi ya kutufanya kuwa wamoja wakati wote na kutufanya taifa la mfano kwa mataifa mengine,jamani sisi ni kisiwa cha amani,tusiichezee amani tuliyonayo leo.
 
Niwaombe tu kuwa Dini zetu leo zisitufikishe mahali ambako kesho tutajuta,badala yake tuzidi kupendana na kumaliza tofauti zetu kwa mazungumzo,najua sio lahisi kujua athari za yale yatakayotokea baada ya kupigana vita,ila baada ya kupigana ndiyo tutajua athari yake,nawaombeni chondechonde watanzania tusifikirie kufika huko,kama ilivyo kawaida yetu huwa tunakaa poamoja na kuzungumza basi hata leo tuzungumze ili kuitunza na kuienzi Amani yetu.Naweza nisieleweke ila natamani kila mmoja anielewe kwa kuwa naipenda Tanzania na watu wake ikiwa ni pamoja na wewe bila kujali dini zetu ama kabila.Tuzidi kumwomba Mungu atulinde na atuepushe na haya yote yanayojitokeza leo na kupoteza umoja wetu na mshikamano.
 
 Pia tujifunze kwa waliotutangulia kupigana vita hasa vya kubaguana kwa sababu ya imani zao au kabila zao.
Shime watanzania tujaribu kusameheana kwa yote na tuanze upya kuitengeneza Tanzania yetu ya siku za nyuma.
MUNGU IBARIKI TANZANIA,NA WATU WAKE.
 
 Rafiki bado nakuombea Mungu akubariki
PAMOJA kwa UMOJA

ABEDDY NGOSSO/SARA K

FANUEL SEDEKIA NA UPENDO WA YESU-MUNGU AKUBARIKI