JE!!! NINI KIFANYIKE FURAHA YA KWELI UIPATE??
Watu
wengi wanapopata matatizo huwa hawakubali kuyapokea. Kuna mfano wa mtu mmoja
ambaye alikuwa bosi katika kampuni, siku moja uongozi wa juu uliamua kumshusha
cheo kutoka ukurugenzi hadi mpokea wageni. Bosi huyo alipotelemshwa cheo kwa
kiwango hicho hakujiona duni kwa wafanyakazi wenzake, badala yake alichofikiri
yeye ni kwamba watu wote wanamuunga mkono na kumsikitikia kwa unyama huo wa
kushushwa cheo kupitiliza.
Zile
fikra za kuhurumiwa na watu zilimfanya awe na furaha na akawa mtu wa kuwahi
kazini kila siku ili watu wakamuone na kumsikitia, jambo ambalo aliamini kuwa
uongozi uliomshusha cheo ndiyo unaopata aibu mbele ya jamii na wala sio yeye.
Kitendo hicho cha kuwahi kazini na kuonekasna ni mtu mwenye furaha kilimfanya
awe mtu wa pekee kwenye jamii, aliweza kutengeneza maswali mengi kwa watu na
hatimaye minong’ono ya kuonewa ilianza kusikika.
Kilichotokea
hatimaye, kampuni moja kubwa ilipata habari ya kuwepo kwa mtu wa aina hiyo,
ikafanya mawasiliano naye na kumwajiri, bila kujali kashfa zilizokuwa
zimemwengua katika wadhifa wake wa kwanza. Jamaa huyo alipopata ajira mpya
alijirekebisha makosa yake ya kugushi na wizi kwa vile alikuwa amejifunza
kilichokuwa kimempata. Bosi huyo aliweza kuendesha kampuni hiyo kwa mafanikio
makubwa, jambo lililowafanya wakuu wake wa zamani wajute kumuondolea wadhifa.
Hapa
tunajifunza kuwa tunapopata matatizo kinachotufanya tupoteze furaha ni fikra
zetu, lakini tukijua kucheza nazo na kuzielekeza katika mlango wa pili,
tunaweza kuyatumia matatizo yetu kupata furaha pia. Lazima kila mmoja wetu
atambue kuwa matatizo ni shule, tunapoyapata tunajifunza. Lakini hatuwezi
kujifunza tukiwa na msongo wa mawazo, lazima tufanye unafiki fulani wa kimawazo
kama alioufanya bosi aliyeshushwa cheo, yeye hakuangalia wadhifa wake wa
zamani, wala namna gani watu wanamtazama katika kazi yake mpya. Mawazo
yanawezaje kutuletea furaha?
Katika
hali ya kawaida hakuna mtu hata mmoja anayeweza kumwambia mwenzake lia naye
akafanya hivyo. Kila siku tunaona na kusikia mengi kutoka kwa ndugu,
rafiki, waalimu wahubiri, wachungaji mapadri wetu na hata kwenye vyombo ya
habari, lakini kusikia huko hakuna maana kuwa ni lazima kutuondolee furaha,
kwani ndani ya akili zetu kuna kitu muhimu ambacho ni maamuzi yetu.
Utawala
wa mawazo yetu ni kazi ya kila siku na uamauzi wa nini ha kufikiri ni suala
ambalo lipo kwenye uwezo wa mwanadamu mwenyewe. Ingekuwa ni lazima kila wazo
baya tunaloliona na kulisikia lazima lituhuzunishe basi tusingekuwa na furaha
hata kidogo katika maisha yetu, kwani hakuna siku ambayo itapita bila kuona, kusikia
au kutendewa jambo baya na mtu mwengine.
Ajali
zinatokea kila siku, watu wanakufa, wanaugua, wanateseka, wanalia, wanaomboleza
na kufanyiana hila, lakini kwa nini hatuyachukulii matukio yote kwa uzito sawa
kiasi ha kulia? Ni kwa sababu tuna uhuru wa kuchagua tulie kwa sababu ya nani
na kwa nina? Na hii ndiyo silaha pekee ya kuyatumia mawazo kutuletea furaha.
Yaani kuchagua lipi la kutuliza na lipi la kutufurahisha na mwisho wa yote tuna
uwezo wa kuyatumia mawazo yetu kuchagua mambo ya kufurahisha na kuyapa
kipaumbele, bila kujali ni mema au mabaya. (Kumbuka mfano wa bosi aliyeshushwa
cheo).
Hivyo ni vema
wakati tunapokuwa na mawazo ndani yetu tukazingatia misingi ifuatayo ambayo
inaweza kutusaidia kufikia uamuzi sahihi juu ya kila tunaloona na kulisikia,
ili mawazo yasitufanye tuhuzunike na badala yake tufurahi. Kwanza ni kujipenda
wenyewe. Tukijipenda hatutajihukumu na kujiona duni mbele ya wenzetu na hivyo
kutopoteza furaha. Pili ni kujiamini, kuamini huku kutatuwezesha kuwa na
msimamo juu ya maamuzi ya kila tunachoshibishwa ndani ya mawazo yetu kupitia
mawasilia ya sauti na yasiyo na sauti.Tatu, kumiliki mawazo yetu yasichukuliwe na ukubwa au
udogo wa tatizo. Udhibiti huu lazima uyaone mambo yote yanayoingia kichwani
kuwa ni ya kawaida kwa vile yapo duniani na yanawakuta watu kama sehemu ya
changamoto za kimaisha. Katika hali ya kawaida ukubwa au udogo wa tatizo
unatokana na mawazo ya mtu husika. Nne, kuwa na uvumilivu juu ya kila jambo kwa
imani kuwa hakuna marefu yasiyokuwa na ncha. Tano na mwisho ni kuhakiki maamuzi
yako kama yako sahihi kabla na baada ya.
Rafiki bado nakuombea Mungu akubariki
PAMOJA kwa UMOJA