KARIBU

KARIBU UPATE HABARI MBALIMBALI KUPITIA BLOG HII;;pamojakwaumoja2012.blogspot.com.
AU PIGA simu 0715408566 kwa Ushauri na maoni

KAULI MBIU/SLGN


HOPES

Friday, July 27, 2012

UJIO MPYA WA MWIMBAJI NA MTANGAZAJI WA PRAISE POWER REDIO

MTANGAZAJI NA MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI VICTOR ARON AL MAARUFU MZEE WA FARAJA TIME AMEKUJA NA SURA MPYA YA ALBAM IITWAYO 2 X 2= 4 NA TAYARI KWA SEHEMU KUBWA IMEKAMILIKA.

Victor Aron
Mtangazaji huyu na mwimbaji wa ni nyimbo za injili amekuwa na nyimbo nyingi zenye ujumbe mkubwa sana kwa kanisa,yaani waumini wote wa dini za ki kristo,upatapo muda ukasikia nyimbo zake utathibitisha hili kwa utunzi wake na ushairi kuwa ni wa watofauti kidogo na tungo  nyingine ulizozizoea.Katika albamu hii mpya kuna vionjo tofauti tofauti yaani zoukrhumba,taraatibu(slow) na nyingnezo.
Watumiaji wa madawa ya kulevya(vijana).

Mwimbaji huyu amekuwa akiimba nyimbo za kuasa sana na watu kumrudia Mungu hasa katika nyakati hizi tulizo nazo,amekuwa akitia moyo sana na kufariji watu walio kata tamaa katika maisha yao ya kimwili na hata kiroho pia.
Mama akichota maji ya shimo
Katika moja ya huduma aliyonayo Victor Aron tofauti na uimbaji pia ni mwenye kutia moyo na kufariji waliovunjika moyo na kukata tamaa na maisha,kwa mtu asiyemfahamu atakuwa ni mgeni katika hili lakini kwa msikilizaji wa praise power redio 99.2 fm atakuwa ananielewa kwa kuwa ni mtangazaji aliyedumu katika kipindi cha faraja time kwa muda mrefu sana zaidi ya miaka mitano(5),hii inamaanisha ya kuwa anakidhi haja ya wasikilizaji wa redio hasa faraja time,kipindi hiki huwa kinaanza saa nne(4)kamili usiku kila siku mpaka saa nane kamili usiku.
Victor Aron mwenye shati la kitenge akicheza na Martha Mwaipaja katika send off pary yake katika ukumbi waV.I.P  D.Jubilee,Sambamba na waimbaji wengine Addo Novemba,Bahati Bukuku na kulia mwishoni ni Boni Mwaitege.
Katika Albamu yake hii mpya yenye takribani nyimbo 9 anatamani imfikie kila mtu kwa maana kwamba ujumbe uliomo ndani ni jibu tosha kwa kila atakaye ipata.
Kwa habari zaidi endelea kutembelea mtandao hasa blog hii itakujulisha kila kitu kinachoendelea kuhusu Victor Aron na huduma yake ambayo Mungu amemwitia.Mpaka hapa sina la ziada nikutakie amani ya bwana.

Rafiki bado ninakuombea Mungu akubariki
Pamoja kwa Umoja

PAMOJA KWA UMOJA FASHION INAKULETEA TSHIRT MPYA

TOA MAWAZO YAKO JUU YA TOLEO HILI JIPYA LA TSHIRT ZA PAMOJA KWA UMOJA
Nipigie katika no 0715 408566

Pamoja kwa Umoja @v1


Pamoja kwa Umoja @v2


Pamoja kwa Umoja @m1


Pamoja kwa Umoja @m2


Pamoja kwa Umoja @p1


Pamoja kwa Umoja @p2


Pamoja kwa Umoja @d1


Pamoja kwa Umoja @d2
Rafiki bado nakuombea Mungu akubariki
Pamoja kwa Umoja

ABEDDY NGOSSO/SARA K

FANUEL SEDEKIA NA UPENDO WA YESU-MUNGU AKUBARIKI