KARIBU

KARIBU UPATE HABARI MBALIMBALI KUPITIA BLOG HII;;pamojakwaumoja2012.blogspot.com.
AU PIGA simu 0715408566 kwa Ushauri na maoni

KAULI MBIU/SLGN


HOPES

Monday, August 19, 2013

JE UMEISIKIA HII????

MTU ASIYEJULIKANA AGAWA FEDHA JIJINI DAR ES SALAM
Bajaji wakiwa kwenye foleni kuwekewa mafuta na mtu ambaye hakutaka kujitambulisha

Mwanaume mmoja, ambaye amekuwa akiongozana na maaskari polisi wawili, amekuwa akigawa fedha za bure kwa watu mbalimbali jijini Dar.

Kijana huyo wa makamo, ambaye kwa wiki hii nzima amekuwa akitajwa kwenye radio mbalimbali, aliwalipia bili wagonjwa wote waliokuwa wamelazwa hospitali ya Mwanyamala na Muhimbili, wodi ya wanawake.


Akizungumza na mwandishi wetu,mmoja wagonjwa wa hospitali ya Muhimbili, Subira Juma alisema kijana huyo alikuja hospitali na kuuliza wangapi wanadaiwa halafu akawalipia bili zao na kisha kuondoka zake bila kujitambulisha.


‘Kwa kweli hata mimi sifahamu kijana huyu katokea wapi, lakini sijwahi kuona mtu akitoa hela bila kujuana, na kisha kuondoka bila kusema lolote
 
 alisema Subira.

Wakati huo huo, wasafiri wa daladala nao, hasa ziendazo Mbagala nao wametajwa kunufaika na mgao huo, ambapo wamekuwa wakilipiwa nauli mara kadhaa na mtu huyo.

Mbali na kulipia watu usafiri, kijana huyo pia anatajwa kuwanufaisha madereva boda boda na bajaji kwa kuwawekea mafuta kwenye vyombo vyao vya usafiri.

 
CHANZO JAMBO TZ

Mwenyeezi Mungu amlipe Pepo huyo Kijana inshallah Wanachama Wenzangu Semeni Ameen.

HATIMAYE ALBAMU YA UKO HAPA KUFANYIKA LIVE

MWIMBAJI JOHN LISU SAMBAMBA KABISA NA MKEWE NELLY KAISI LISU KUREKODI LIVE ALBAMU YAO YA UKO HAPA.
 Huyu ndiye John Lisu na mkewe Nelly Kaisi Lisu katika picha ya uzinduzi wa audio albamu ya
 UKO HAPA
 Alipo bwana yote yanawezekana/mahali ni pazuri watu wakiishi kwa upendo bila shaka ndiyo maneno yanayotawala nyuso za watu wote hapa katika picha
 
 Palipo na mafanikio hali kama hii lazima iwepo(UPENDO) Ni John Lisu na mkewe Nelly
 John Lisu akilitendea haki gitaa lake
 Baadhi ya back vocal(Waitikiaji)Katika albamu ya UKO HAPA
 Watumishi wa Mungu Ambao wamekuwa pamoja mara kwa mara na John Lisu katika matamasha.Jaribu kuwapa majina yao kama kweli unawajua?????????
Hili ndilo tangazo rasmi kwaajili ya tamasha la UKO HAPA recordin LIVE
Tamasha hili litafanyika katika ukumbi wa CCC UPANGA, Tayari tiketi zinzpatikana DPC Kinondoni,Tarakea Mwenge duka la Cd na Mbogo Shop Kariakoo.Wahi sasa usije kosa tiketi za tamasha hili.





Usipange kukosa kumwabu Mungu katika roho na kweli
MUNGU KWANZA
Mungu ibariki Tanzania na watu wake wote

ABEDDY NGOSSO/SARA K

FANUEL SEDEKIA NA UPENDO WA YESU-MUNGU AKUBARIKI