KARIBU

KARIBU UPATE HABARI MBALIMBALI KUPITIA BLOG HII;;pamojakwaumoja2012.blogspot.com.
AU PIGA simu 0715408566 kwa Ushauri na maoni

KAULI MBIU/SLGN


HOPES

Friday, July 13, 2012

UNCLE JIMMYTEMU BLOGSPOT.COM

NI USIKU WA UNCLE JIMMY TEMU KUTIMIZA MWAKA MMOJA WA BLOG YAKE

 Huyu ndiye Uncle Jimmy katika pozi
 Uncle Jimmy akiwa na Anord Kayanda katika moja ya majukumu yake ya blog.
 Uncle Jimmy katika pozi na hii ni moja kati ya picha iliyo katika Tamthilia
 Uncle Jimmy akiwa na mmoja wa wadau wa FOF.
Uncle Jimmy akiwa na marehemu Steven Kanumba katika moja ya majukumu yake. 
Uncle Jimmy akiwa Rebeke Malope katika moja ya majukumu yake
Waswahili walitangulia na Kusema UJANA MAJI YA MOTO na ni Ki-Mungu kumtumikia Mungu siku za UJANA kabla hazijafika siku utakazokuja kusema kuwa siwezi.Man of GOD James Temu ni kijana na Mtangazaji wa kituo cha Redio cha Kikristo Kiitwacho Praise Power cha JIJINI Dar es Salaam, pia Jimmy ni Mcheza Filamu maarufu nchini na on top of it Uncle Jimmy kama ajulikanavyo na wengi ni mmoja kati ya ma-blogger mahiri wa habari za wa Kikristo nchini Tanzania.
Uncle Jimmy akiwa na Ray Kigosi katika moja ya sehemu ya majukumu yake
Mwaka jana mwezi wa saba James Temu alianzisha blog yake iitwayo www.unclejimmytemu.blogspot.com na mwaka huu anatimiza mwaka mmoja katika kuielimisha jamii kwa habari ya ufalme wa Mungu kupitia mtandao.Hivyo basi kwa kuliona hilo gentleman huyu mrefu mweupe mwenye sauti nyembamba ameamua kuwaalika wadau wote kwenye Coctail Party maalumu ya kumshukuru Mungu kwa kumuwezesha kutimiza mwaka mmoja.
Uncle Jimmy akiwa katika harakati za kucheza Filamu pamoja na Ray na Waridi
Shughuli nzima itafanyikia tarehe 20.07.2012 katika Tamaal Hotel iliyoko maeneo ya Mwenge nyuma ya kituo cha Polisi, katika usiku huo marafiki ndugu na jamaa watapata nafasi ya kumfahamu Jimmy alikotoka alipo na mataraji yake ya hapo baadaye.Muda ni kuanzia saa 1:00 usiku mpaka 3:00 usiku kiingilio ni BURE.Kama uko Dar es Salaam hii si ya kukosa fika Tamaal na tuseme EBENEZER pamoja na mwanahabari huyu.
Sambamba na Kumfahamu Jimmy,kwa kila atakayefika atapata nafasi ya kumtukuza Mungu LIVE pamoja na Live Band kutoka kwa Dar es Salaam Gospel Band pamoja na wanamuziki wengine maarufu nchini.Katika usiku huo chakula kitatolewa bure kwa kila atakayefika ambapo watangazaji wengi maarufu nchini watakuwepo katika kumshukuru Mungu pamoja na mwanahabari mwenzao.Kwa ROHO SAFI tukutane pale Tamaal Hotel ijumaa ya wiki ijayo(20.07.2012) tuseme EBENEZER pamoja na James Temu

Rafiki yangu bado nakuombea Mungu akubariki
Pamoja kwa umoja.

ABEDDY NGOSSO/SARA K

FANUEL SEDEKIA NA UPENDO WA YESU-MUNGU AKUBARIKI