AJALI MBAYA YA MV STAR GATE IMEZAMA MAJI KATIKA BAHARI HINDI
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk
Mwinyihaji Makame akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari kuhusiana na kuzama kwa Meli ya Star Gate hukokatika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.
Meli ya Mv. Star Gate imezama karibu na Kisiwa cha Chumbe ambapo watu 12 wamefariki kwa taarifa toka kwa watu walioko eneo la tukio, na wengine kadhaa wamejeruhiwa.
Akitoa taarifa fupi kwa waandishi wa habari,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini alisema taarifa za kuzama kwa meli hiyo ilitolewa na Boti iendayo kasi ya Kilimanjaro III iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kwenda Zanzibar ndipo ilipoiona meli hiyo ikizama.
“Tulipata taarifa kutoka Boti ya abiria ya Kilimanjaro III saa 7:50 mchana waliporipoti kuona meli ikizama karibu na Kisiwa cha Chumbe” Alisema Waziri Mwinyihaji.
Waziri huyo alisema Meli hiyo imezama maili sita kuelekea Kisiwa cha Yasin Kusini mwa Kisiwa cha Chumbe kilichopo Unguja maili kadhaa kutoka Bandari ya Malindi.
Waziri Mwinyihaji alisema idadi ya abiria walikuwa 250 ambao ni watu wazima, watoto 31 na mabaharia 6. “Tumepeleka waokoaji, kuna boti tano zipo eneo la tukio kushirikiana na waokoaji wengine” Alisema Waziri Mwinyihaji.
Alisema maiti zote zitapelekwa viwanja vya Maisara Zanzibar kwa ajili ya ndugu na jamaa kuzitambua maiti za ndugu zao ambapo majeruhiwa wote watatibiwa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja.
Miongoni mwa abiria waliookolewa ni raia 13 wa Mataifa mbalimbali ya nje huku raia mmoja ambaye hakuweza kutambuliwa utaifa wake amepoteza.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akiwa katika Eneo la Bandari akishuhudia kuletwa kwa majeruhi mbalimbali waliookolewa katika meli ya Star Gate iliozama huko katika eneo la Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.
Poleni sana watanzania wenzangu.
Poleni sana sana watanzania wenzangu jambo hili limetushtua wote.
Ni majonzi tu katika eneo hili lote
Jeshi kikosi cha KMKM kikiwajibika katika uokoaji.
Kazi ya uokoaji majeruhi ikiendelea chini ya jeshi chini ya kikosi cha KMKM.
Wazamiaji kutoka Kikosi cha KMKM pamoja na Jeshi tayari wapo eneo la ajali kusaidia kuokoa maisha ya wananchi waliokumbwa na maafa haya.
Wanachi na jeshi la KMKM wakiendelea kusaidiana kuokoa majeruhi wa Mv Star Gate.
Majonzi majonzi kwa wakazi wote wa eneo la tukio.
Wananchi mbalimbali wakishuhudia tukio la kuokolewa watu waliozama na meli ya Star Gate huko katika hukokatika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.
Majonzi yatanda katika eneo la tukio,wananchi hawaamini kilicho tokea si wa mama,si wababa wala watoto ni majonzi na huzuni
Ndugu na jamaa wakifarijiana na kulia juu ya msiba huu wa ndugu na wapendwa wao kufia majini na wengine majeruhi
Meli ya Mv Skagit iliyokuwa safarini kutoka Dar kuelekea Zanzibar imezama majira ya saa nane mchane hivi leo katika maeneo Pungume na Chumbe baada ya kukumbwa na upepo mkali.
Meli hiyo inayosadikiwa kuwa na abiria 250 inasemekana imepindukia upande mmoja na huku abiria wengi wakiweza kuokolewa kutokana na jitihada mbali mbali kupitia vile vile msaada wa boti za Mv Kilimanjaro, Tug ya Bandari na vyombo vyengine.
Meli ya Mv Skagit iliyokuwa safarini kutoka Dar kuelekea Zanzibar imezama majira ya saa nane mchane hivi leo katika maeneo Pungume na Chumbe baada ya kukumbwa na upepo mkali.
Meli hiyo inayosadikiwa kuwa na abiria 250 inasemekana imepindukia upande mmoja na huku abiria wengi wakiweza kuokolewa kutokana na jitihada mbali mbali kupitia vile vile msaada wa boti za Mv Kilimanjaro, Tug ya Bandari na vyombo vyengine.
Kwa niaba ya watanzania wenzangu ninatoa salamu za pole kwa ndugu,jamaa na wote juu ya msiba huu wa watanzania wenzetu walio kufa maji,pi Mungu baba awape moyo wa amani katika kipindi hiki kisichozoeleka.poleni sana poleni.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
Rafiki yangu bado ninakuombea Mungu akubariki
Pamoja kwa Pamoja