KARIBU

KARIBU UPATE HABARI MBALIMBALI KUPITIA BLOG HII;;pamojakwaumoja2012.blogspot.com.
AU PIGA simu 0715408566 kwa Ushauri na maoni

KAULI MBIU/SLGN


HOPES

Sunday, September 23, 2012

MAHALI NI PAZURI NDUGU WAKAAPO KWA AMANI

PAMOJA KWA UMOJA
(ERICK BRIGHTON) NAPENDA KUKUSALIMU KATIKA JINA LA YESU KRISTO,POPOTE PALE ULIPO NDUGU,JAMAA AU RAFIKI.NDUGU MPENDWA KATIKA BWANA NINAPENDA  KUKUSHIKISHA BARAKA ZA BWANA KATIKA TAMASHA KUBWA MWISHONI MWA MWEZI WA KUMI.

ERICK BRIGHTON
Mpendwa popote pale ulipo napenda kukusalimu tena katika jina la yesu kristo kupitia ukurasa huu.Napenda kukushirikisha katika moja ya nguzo kubwa katika ufalme wa Mungu kwa kukutanisha wewe na wateule wenzako mahali pamoja na kumtukuza yeye kwa kusifu na kuabudu pamoja,pia napenda nikushirikishe katika jukumu katika tamasha hili la kujiona kuwa wewe ni mmoja kati wa watu ambao ni muhimu sana Mungu amewakusudia,mara nyingi tumeshindwa kumwona Mungu katika maisha yetu ya kila siku kwa sababu nyingi ikiwa ni pamoja na kujihisi kuwa sio walengwa waliokusudiwa.
 
Kwa muda mrefu nimekuwa na mzigo wa kumtumikia Mungu sana na moja kati ya mzigo nilionao ni kwa vijana wenzangu kuwaweka mahali pamoja wakimtumikia MUNGU nakutoka katika mateka ya ibirisi shetani,ila nimekuwa nakutana na changamoto kubwa ikiwa ni pamoja na wengi kuto kujitambua na mengine kama hayo.Nimekuwa najisikia vibaya sana pale napoona vijana wanatoka makanisani kumwimbia Mungu wao badala yake wana kimbilia kuimba miziki ya kidunia,ukweli hili limekuwa ni moja kati ya jambo ambalo linaniumiza sana.Katika kuliona hilo niliamua kuanza kujitolea kwa kuwawezesha wasio na uwezo(pesa) za kurekodi wenye uwezo wa kumwimbia Mungu katika roho na kweli na kufanikiwa kuwapata,kiu yangu haikuishia hapo bado nikaona ninaom uwezo wa kuwa sababishi ya watu kumrudia Mungu na kuanzisha Bendi ya vijana ikiwa ambayo mpaka sasa ina miezi miwili tu,mpaka sasa.
 
MATARAJIO NA MALENGO
Matarajio na malengo yangu ni kuwafikia vijana mahali popote pale walipo ili kumtumikia Mungu wakati huu wa ujana wao,pia kuondoa tatizo kubwa na kilio juu ya ajira.Baada ya kufanikiwa kuipata bendi nimeona niwakati sasa kupitia ROHO MTAKATIFU wa kuizindua bendi hii ambayo mpaka sasa haina jina ila nimatumaini yetu kwa wewe ndiye uliye na jina la bendi hii.Hivyo mnamo mwezi wa kumi Tunatarajia kufanya uzinduzi mkubwa wa kuitambulisha bendi na shughuli zote zitakazokuwa zinafanywa na vijana wa pamoja kwa umoja ikiwa ni pamoja kuwapa nafasi kupata semina za neno la Mungu,semina za saikolojia,semina za ujasiriamali na kazi za Utangazaji redioni,Mc,Utayarishaji wa muziki(Producer) na kazi zote zinazohusu mambo ya Graphics michoro na kuprinti Tshirt na matangazo ya aina zote.
Erick Brighton(kulia)na Silas Mbise(kushoto) katika pozi la pamoja.
 
TAMASHA HILO:
Tamasha hilo litakuwa ni la live la kwanza kunyika katika ardhi ya Tanzania kwa kukusanya waimbaji wengi kwa wakati mmoja katika jukwaa moja,itakuwa ni Bendi za live nane na kwaya tano toka sehemu mbalimbali
na waimbaji wakujitegemea wa nne.Japo nafasi bado ipo kwa bendi itakayokuwa inapenda kushiriki katika Tamasha hili.Kila kitu kimesajiriwa.
 
OMBI LANGU KWAKO MWANA WA MUNGU :
Baada ya kuona na kujifunza mambo mbalimbali ambayo yamekuwa yakisababisha matamasha mengi kuharibika na kuzorota nimeona nikushirikshe katika baraka hizi kwa wewe kutupigia simu kupitia namba 0715408566 kwa ushauri mzuri wenye lengo la kumwinua kristo na si kumwaibisha.Tamani kushiriki sehemu yoyote ya baraka ili kufanikisha tamasha hili,moja kujitoa kwa chochote kile ambacho Mungu amekubariki,kumbuka waimbaji watakuwa zaidi ya 150 na kunauwezekano wa tamasha hili kufanyika siku mbili mfululizo jumamosi na jumapili.Kuanzia hapa utakapo soma ukurasa huu naomba kama upenda kwa kumshirika roho mtakatifu akupe uwezo wa kufunga na kuombea tamasha hili maana linakwenda kuibadilisha Tanzania yetu,litakwenda kufuta mateja,machangu doa na mengine hayo yote yenye kufanana na haya.
KWA YEYOTE AMABAYE ANGEPENDA KUSHIRIKI PAMOJA NASI ANAWEZA KUPIGA SIMU HII
 0715-408566 PIA Email erick.brighton45@gmail.com.
  
ANGALIZO
Mwenye nia ya kushirikiana nasi kwanza awe na hofu ya Mungu tusingependa mwenye nia ya kutaka umaarufu kupitia kumtumikia Mungu bali awe na mzigo na uchungu na vijana na taifa kwa ujumla,yote kwaajili ya bwana.
Vile vile matangazo mbalimbali kuhusu tamasha hili utayasikia katika vyombo vya habari kuanzi wiki ya pili ya mwezi ujao wa kumi.
MUNGU AKUBARIKI SANA POPOTE PALE ULIPO
KWA MAELEZO ZAIDI PIGA 0715 408566

ABEDDY NGOSSO/SARA K

FANUEL SEDEKIA NA UPENDO WA YESU-MUNGU AKUBARIKI