KARIBU

KARIBU UPATE HABARI MBALIMBALI KUPITIA BLOG HII;;pamojakwaumoja2012.blogspot.com.
AU PIGA simu 0715408566 kwa Ushauri na maoni

KAULI MBIU/SLGN


HOPES

Wednesday, September 5, 2012

KESI INAYOMKABILI ASKOFU STANLEY HOTAY

MAHAKAMA KUU KANDA YA ARUSHA IMEITUPILIA MBALI KESI DHIDI YA ASKOFU STANLEY HOTAY
 
Askofu Stanley Hotay wa kanisa la Anglikana dayosisi ya mount Kilimanjaro
Hapa Askofu Stanley Hotay akiwa nchini Uingereza na The worldwide Family
Mahakama kuu kanda ya Arusha imetupilia mbali kesi iliyofunguliwa na waumini watatu wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mount Kilimanjaro(MDK)ya kumpinga Askofu Stanley Hotay kuwa askofu wao.
 
Katika  hukumu hiyo jana,Jaji Fatuma Massengi alikubaliana na pingamizi zilizowasilihwa mahakamani hapo na mawakili wa utetezi kuwa  mahakana haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo kwa sababu kanisa lina katiba yake na walipaswa kupeleka ngazi ya kanisa kabla ya kukimbilia mahakamani.
 
Chanzo ni gazeti Habari leo.
 
Rafiki bado nakuombea Mungu akubariki
PAMOJA kwa UMOJA

AJALI MBAYA YAMPATA MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI

AJALI MBAYA ILIVYOTOKEA MAENEO YA TULA MKOANI TABORA NA KUSABABISHA MAJERAHA KWA MUIMBAJI WA MUNGU
 SIFA JOHN,WATU WENGINE WAPOTEZA MAISHA.
Imetokea leo hii.

 
Huyu ndiye Sifa John ambaye amepata ajali na kupata majeraha kichwani na sehemu nyingine za mwili wake,ajali hii ilitokea maeneo ya Tula mkoani Tabora akielekea kwenye huduma ya uimbaji
 
 
Picha hii Sifa John akihudumu katika tamasha la uzinduzi Albam mti wenye matunda ya mwimbaji mama mchungaji Deborah Said wa jijini Dar es salaam.
Sifa John (kushoto) akishuhudia uzinduzi wa albamu mti wenye matunda ya Deborah Said(kulia)
 
Waweza sikiliza mahojiano kati sifa John na pamojakwaumoja njinsi ambavyo safari yao toka Dar kuelekea Tabora ilivyokuwa mpaka ajali inawapata katika eneo hilo la Tula mkoani Tabora.
Wapendwa popote mlipo tuzidi kuwaombea kwa Mungu awape uzima na afya wote walio patwa na ajali hii.Zaburi 23;4

Rafiki bado nakuombea Mungu akubariki
PAMOJA kwa UMOJA
 
 

ABEDDY NGOSSO/SARA K

FANUEL SEDEKIA NA UPENDO WA YESU-MUNGU AKUBARIKI