KARIBU

KARIBU UPATE HABARI MBALIMBALI KUPITIA BLOG HII;;pamojakwaumoja2012.blogspot.com.
AU PIGA simu 0715408566 kwa Ushauri na maoni

KAULI MBIU/SLGN


HOPES

Friday, October 5, 2012

HII NI KWA WALE WALIOTAMBUA KUSUDI LA MUNGU

KUMTUMIKIA MUNGU NI WITO NA BILA KUUCHOCHEA WITO HAUWEZI KULIFIKIA KUSUDI LA MUNGU.TUNATARAJIA KUWA NA TAMASHA KUBWA SANA AMBALO LITAFANYIKA MWISHONI MWA MWEZI HUU WA 10 NA AMBALO LITAKUWA NA JINA LA GOSPEL FESTIVAL.
Bonyeza play usikilize nyimbo inayokuunganisha wewe na wapendwa wenzako

ERICK BRIGHTON
Napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa wote walioguswa na taarifa hii kwa mara ya kwanza nilipo itoa na kuweza kunipigia simu na wengine kunitumia ujumbe mfupi wa kunitia moyo na kuendelea kuliombea tamasha hili,pia nawashukuru na kuwapa pole wote ambao kwa namna moja ama nyingine wamenitafuta na hawakunipata kwa simu na email.
Dhumuni la mimi kuendelea kukushirikisha ni kutaka nawe upate baraka za bwana na kuliweka mahali pengine kanisa na taifa letu la Tanzania,nimeona ni vyema na wewe ukashiriki kwa sehemu yako katika tamasha hili na kuondoa dhana ya mashindano katika kumtukuza Mungu.Tamasha hili ni kubwa sana kutokana na uwingi wa watumishi/waimbaji wa bendi na kwaya na waimbaji binafsi ambao jumla yao ni 200 na watumishi wengine wengi kutoka sehemu mbalimbali,ndiyo maana nimeona nikushirikishe na wewe uweze kushirikiana na mimi katika hili tukinia mamoja ya kulitoa mahali fulani taifa letu la Tanzania.
 
Katika tamasha hili kutakuwa na viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali na viongozi wa serikali mawaziri na wabunge na viongozi wengine lengo ikiwa ni kusifu na kuabudu pamoja na kulitoa taifa letu katika majanga na mateso mbalimbali.Hivyo kwa wewe ambaye utaguswa kushirikiana na mimi na wengine waliojitokeza bado tunahitaji wanakamati wa tamasha hili.Pili bendi zote na kwaya zote ningependa kuwakumbusha kufanya mazoezi makali ili kukidhi haja ya wadau watakao jitokeza mahali pale.
 
Tamasha hili ni la live mwanzo hadi mwisho.
Kwa mawasiliano zaidi nipigie katika namba hii
0715 408566 au Email:erick.brighton45@gmail.com
Epuka kuishi kimazoea,ishi kwa hofu ya Mungu kumbuka duniani tunapita tu!
MUNGU AKUBARIKI POPOTE PALE ULIPO NAKUPENDA
Rafiki bado nakuombea Mungu akubariki
PAMOJA kwa UMOJA

ABEDDY NGOSSO/SARA K

FANUEL SEDEKIA NA UPENDO WA YESU-MUNGU AKUBARIKI