KARIBU

KARIBU UPATE HABARI MBALIMBALI KUPITIA BLOG HII;;pamojakwaumoja2012.blogspot.com.
AU PIGA simu 0715408566 kwa Ushauri na maoni

KAULI MBIU/SLGN


HOPES

Friday, September 21, 2012

DARASA HURU LA UFAHAMU


JE WAJUA ROHO YAKO NI MAKAO MAKUU YA MUNGU NA MWILI WAKO NI NYUMBA YAKE YA  SALA
Huu ndiyo MOYO wa mwanadamu.
Je nini kusudi la haya yote!!!?Hivi ndivyo kwenda na wakati au wasiovaa ni washamba.TAFAKARI!sana huu ni mwanzo ila Mwisho wake ni mmbaya zaidi.tafakari !!!
Nikweli maisha ni magumu na changamoto ni nyingi kila itwapo leo,Je umeshawahi jiuliza kwanini Mungu kakuumba na kwanini mpaka leo uko hai!!? Yawezekana ndiyo au hapana,mimi leo natamani ujiulize na hapa ndipo utakuwa mwanzo wa mabadiliko ya maisha yako baada ya kutambua kusudi au dhumuni la Mungu juu yako.Mara nyingi tunapokuwa na maisha ya furaha huwa si rahisi kukumbuka kuna Mungu au kuwa Mungu ndiye sababbishi la hayo maisha mazuri wengi hufikia kuamini kuwa ni wao ndiyo sababu ya mafanikio yao si Mungu.Naomba nizungumze na wewe ambaye unaishi maisha ya starehe bila hofu ya Mungu na wakati mwingine hutaki hata kusikia chochote kinachomhusu Mungu,Je ni kweli unasikia lakini usikii au unaona lakini hauoni kile amabcho Mungu anataka usikie au kuona!?Kwanza natamani utambue kwa haya yote yanamwisho wake na mwisho wake ni mbaya sana natamani sana leo uwe ni mwisho wa mabaya yote na iwe siku mpya kwa kwa kuishi maisha ya Mungu kwa kuwa umamwakilisha Mungu hapa duniani.Jaribu kuepuka kuongozwa na hisia maana zitakutawala mpaka fikra zako,kwa kawaida hautakiwi kuongozwa na kutawaliwa na hisia bali tunatakiwa kuongozwa na kutawaliwa naufahamu hasa wa neno la Mungu.
 
Kwa akili tu! ya kawaida kweli kweli hapa unaonyesha nini mbele za Mungu ni kweli kabisa Mungu anajivunia wewe kwa uvaaji huu?ni kweli huku ndiko kwenda na wakati!?
Jitahidi kuepuka mambo ya msingi ambayo yanasababisha maisha yako yawe mbali na Mungu pia itambue dhambi na baada ya kuitambua dhambi tambua kusudi la aliyeileta dhambi katika maisha yako na nini kusudi lake kukuletea dhambi.Kumbuka wewe ni kama uwanja wa ndege Mungu anakutumia ili makusudi yake yapate kutua kupitia wewe,kakupa uwezo wa kutambua jema na baya hivyo tamani kufanyika uwanja wa Mungu kutua kwako na kushusha ndege zake.
 
Epuka kupotezwa na mabadiliko ya wakati yaani teknolojia na vitu vinginevyo kama mazingira.Tamani kujua kusudi la Mungu kuleta teknolojia hizi za mitandao ya Computer na simu,usipojua utajikuta anayakubali mabadiliko kwa kupotea kwa mfano kutumia mitandao ya kijamii Facebook,Tweter,Viber,Whatsapp na Blog isivyo,tamani hiyi vyote vifanyike madhabahu ya Mungu kukutana na watu wake.
 
Kutokana na haya yote na mengine mengi ambayo wewe mwenyewe ndani mwako umeona yatosha kuishi maisha yasiyo mpendeza Mungu na unahitaji kumpatia bwana yesu maisha yako ungana na sala hii ya toba hapa chini.
Bonyeza play hapa chini



 
 
 
Rafiki bado nakuombea Mungu akubariki
PAMOJA kwa UMOJA

ABEDDY NGOSSO/SARA K

FANUEL SEDEKIA NA UPENDO WA YESU-MUNGU AKUBARIKI