JINSI GANI KUTOKU JIHESHIMU KUNAVYOWEZA KUKUNYIMA FURAHA!!
Ni
muhimu kila mtu akaishi kama yeye alivyo, lakini linapokuja suala la
kuchangamana na ulimwengu, lazima kuwe na kitu cha kujifunza kwa sababu huwezi
kuishi nje ya familia na watu wengine.
Kwa
msingi huo ili mtu aweze kupata furaha lazima afahamu namna atakavyoweza
kujisahihisha tabia yake kwa kujiheshimu yeye na kuwaheshimu wengine anaoishi
nao. Kwa maana kuishi kama mtu anatakavyo bila kutazama wengine ni jambo
baya. Hivyo dokezo zifuatazo ni muhimu kwa kila mtu kuzifahamu ili kuondoa
mkwaruzano kati ya mtu na mtu.
A
–Wafanyie wengine mema
Furaha
haiwezi kuja kama mtu hajiheshimu mwenyewe na kuwafanyia wengine mema ambayo
angependa atendewe. Watu wengi wamekuwa hodari kutembea na wake za watu, kuiba,
kudhuru, kutukana, kudharau wengine na hata kunyanyasa, bila kugeuza upande
wapili wa shilingi na kufikiri endapo wangefanyiwa wao hali ingekuwaje, si
wangepoteza furaha? Sasa kama jibu ni ndiyo kwa nini wao wawe mahodari
kuwaumiza wengine? Ni wazi kwamba kila mwanadamu angekuwa makini kufanya yale
ambayo angependa kufanyiwa, kiwango ha huzuni kingepungua, na hii ndiyo
changamoto kubwa kwa mtu atakaye kupata furaha lazima awafanyie wengine wema
kwanza kabla ya yeye kufanyiwa.
B
– Kuwa kiongozi
Katika
maisha kuna watu ambao hawaelewi kuhusu matumizi ya mawazo na namna ya kutenda
kama binadamu, hivyo kwa wale ambao wanaelewa nini maana ya maisha ni vema
wakawa viongozi kwa wengine, viongozi katika kusamehe, kukubali kosa, kutenda
haki na kusimamia ukweli.
C-
Kushukuru
Ni
watu wachache sana ambao hushukuru wafanyiwapo mabaya, lakini inashauriliwa
kwamba ili kuuita furaha na kupunguza nguvu ya huzuni ni bora mtu akajifunza
kushukuru hata kama amefanyiwa jambo baya.
D
- Kuwa na juhudi
Mambo
yote tunayoyafanya lazima ambatane na juhudi. Ikiwa tunatafuta majibu ya nini
tunataka kifanyeke katika kupata furaha lazima tuwe na bidii, tusifanye vitu
kwa uzembe kwani matokeo yake ni kushindwa ambako kutatuingiza katika shida
ambazo zitatuhuzunisha. Umeolewa jitahidi kulinda ndoa yako, jitahidi katika
kazi na kila jambo ili usikwame.
E-
Kuchunga ulimi
Kuna
watu wengi ambao wanapoteza furaha kwa kutojua namna ya kutumia ndimi zao.
Utakuta mtu yuko katika kati ya watu, anatukana na wakati mwingine kutamka
maneno ambayo wenzake hayawapendezi. Kujiheshimu ni pamoja na kuchuja maneno ya
kusema mbele za watu kulingana na mahitaji yaliyopo, kuropoka ropoka kuna
madhara. Kabla hujasema kitu tafakari kama usemecho kitaleta furaha au huzuni.
Tamani sana Mungu akupe hekima katika maisha yako ya kila siku na hesima ya Kimungu na heshima,kumuheshimu kila mtu unayemfahamu na hata usiyemfahamu.
Rafiki bado nakuombea Mungu akubariki
PAMOJA kwa UMOJA