Rais wa Ghana John Attah Mills afariki
25 Julai, 2012 - Saa 17:51
Taarifa kutoka afisi ya rais zinasema kuwa alifariki
ghafla baada ya kupelekwa hospitali siku ya
jumatatu.
Taarifa zinazohusiana
Msaidizi wake pia amethibitisha kufariki kwa
kiongozi huyo.
Kifo cha rais wa taifa la pili duniani kwa ukuzaji wa
cocoa kimekuja wakati alikuwa anajiandaa
kupogania tena urais.
Rais Attah Mills ambaye husafiri mara kwa mara
kwenda ng'ambo kwa matibabu alifariki muda mfupi
baada y kupelekwa katika hospitali moja mjini
Accra , Ghana.
Ni hivi majuzi tu rais huyo alisafiri hadi Marekani
kwa kile kilichosemekana kwa ni uchunguzi wa
kawaida wa afya yake.
Kwa muujibu wa katiba ya Ghana, Makamu wa Rais
John Dramani Mahama anatarajiwa kushikilia
hatamu za uongozi hadi uchaguzi wa urais
utakapofanywa.
Ghana ilikuwa inatarajiwa kwenda katika uchaguzi
mkuu mwezi Disemba mwaka huu ambapo John
Attah Mills alikuwa ametangaza nia yake ya kutete
a uadhifa wake.
Wakati wa uongozi wake, uchumi wa Ghana
uliimarika na demokrasia kupanuka zaidi.
" Ni kwa masikitiko makuu na kwa moyo mzito...
Tunatangaza kifo cha ghafla cha rais wa jamhuri ya
Ghana " taarifa iliyotumiwa shirika la Reuters
kutoka ofisi ya rais ilisema.
Tarifa hiyo ilisema kuwa Rais Mills mwenye umri wa
miaka 68 alifariki saa chache tu baada ya kupelekwa
hospitali.
Hata hivyo hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa.
Lakini msaidizi wake mmoja ambaye hakutaka
kutajwa, alisema kuwa Rais John Attah Millis
alisikika siku ya Jumatatu akilalamika kwa
anaumwa.
Hali yake ilizorota na hatimae kufariki mapema siku
ya Jumanne.
Bwana alitoa,bwana ametwaa.