KARIBU

KARIBU UPATE HABARI MBALIMBALI KUPITIA BLOG HII;;pamojakwaumoja2012.blogspot.com.
AU PIGA simu 0715408566 kwa Ushauri na maoni

KAULI MBIU/SLGN


HOPES

Monday, July 30, 2012

DEBORAH SAID AZINDUA VIDEO YA ALBAM YA MTI WENYE MATUNDA.

VIDEO YA MTI WENYE MATUNDA YA MTUMISHI WA MUNGU DEBORAH SAID YA ZINDULIWA NDANI YAKANISA LA MAISHA YA USHINDI AMBAKO NDIKO MTUMISHI HUYU ANAHUDUMU,CHINI YA MUMEWE MCHUNGAJI JOHN SAID::
Hili ndilo kanisa la maisha ya ushindi ambako uzinduzi umefanyika wa mti wenye matunda wa Deborah Said.

Hili lilikuwa ni tukio la mgeni mtumishi wa Mungu Thomas Mwakalibule kuzindua audio cd akiwa na mtumishi wa Mungu Deborah Said mwimbaji/mama mchungaji

Mgeni akikagua ni jinsi gani teknolojia ilivyotumika katika kuitengeneza Cd hii,tunaona wakicheka kidogo sambamba na Mc wa shughuli hii Douglass Pius mtanagazaji wa redio ya dini Praise Power

Bado mgeni akizitazama kwa makini Cd hizi zenye albamu ya MTI WENYE MATUNDA

Mc wa shughuli hii mtumishi wa Mungu mwimbaji Sifa John akitoa maelekezo fulani katika uzinduzi huu.

Mc wa shughuli hii mtumishin wa Mungu Douglass Pius akimkaribisha mgeni katika madhabahu ya bwana.

Mtumishi wa Mungu mwenyeji mchungaji John Said akiwa na mgeni wake mchungaji Michael Anaki toka huduma yaAkuzamu


Mchungaji Michael Anaki toka huduma ya Akuzamu akizindua Video Cd ya mti wenye matunda.


Tayari kwa ishara hii Video Cd ya mti wenye matunda imezinduliwa rasmi na mchungaji Michael Anaki.

Mtumishi wa Mungu toka huduma hii chini ya mchungaji John Said akitoa neno juu ya utoaji katika shamaba la bwana,anasema unapotoa au kushiriki jambo lolote lenye kumpa Mungu Utukufu basi unakuwa umemkopesha Mungu so hivyo kwako wewe ambaye uko mahali hapa na yeyote yule atakayeona kazi hii kwa njia ya Tv basi anayo nafasi ya kushiriki baraka za bwana kwa kununua kazi hii ya mtumishi wa Mungu Deborah Said albamu ya MTI WENYE MATUNDA.

 KATIKA ENEO LA SIFA alikuwepo Norbert producer kutoka YEHOVA studio inayopatikana makongo juu.



Pia Chris na madam Ruth walikuwepo wakihuduma mahali hapa


Kutoka Kigoma mpaka Dar es salaam kama ambavyo yeye hupenda kusema mara kwa mara anaitwa mtumishi wa Mungu Victor Aron mwimbaji na mtanagzaji toka Praise Power Redio 99.2fm.Ambaye naye albamu yake iko njiani na tena muda si mrefu itakuwa hewani/madukani.

Dhumuni la uzinduzi huu lilikuwa ni kuchangia ujenzi wa kanisa la Maisha ya ushindi linalopatikana Ubungo Extenal na ndiko anakopatikana mtumishi wa Mungu Deborah Said ambaye ni mke wa mchungaji John Said.Milango iko wazi kwa ko wewe ambaye utasikia wito ndani ya moyo ukisema na wewe juu ya kushiri baraka za bwana katika kumtolea yeye katika ujenzi wa kanisa(hema la bwana) au nyumba ya ibada.
Waimbaji wengi walikuwepo ikiwa ni pamoja na Tina Malego,Neema Jekonia na wengine wengi,pia watu walikuwe ni wengi sana tofauti na ambavyo walitegemea wengi.

Rafiki bado nakuombea Mungu akubariki
Pamoja kwa Umoja

No comments:

Post a Comment

ABEDDY NGOSSO/SARA K

FANUEL SEDEKIA NA UPENDO WA YESU-MUNGU AKUBARIKI