KARIBU

KARIBU UPATE HABARI MBALIMBALI KUPITIA BLOG HII;;pamojakwaumoja2012.blogspot.com.
AU PIGA simu 0715408566 kwa Ushauri na maoni

KAULI MBIU/SLGN


HOPES

Sunday, July 29, 2012

NINA MIAKA (20) ISHIRINI SIJAFANIKIWA KUPATA MTOTO(KUZAA)
MAGRETH FRANCIS

Dada Magreth Francis mwenyeji wa Mabibo relini jana jumamosi 28/07/2012 katika kipindi ninacho kiongoza kupitia Praise Power Redio 99.2 fm,ilikuwa ni majira ya saa nane na dakika therathini na sita usiku(saa 8:36 usiku) alinishirikisha juu ya maombi kwa mwenyezi Mungu juu yake kupata mtoto maana yuko katika ndoa miaka 20 hajafanikiwa kupata mtoto

Kama jinsi anavyoonekana dada yetu bado anaamini kwa yesu bado inawezekana kupata mtoto hajakata tamaa.
 Pamoja na yote hayo kuwa ni sehemu ya maisha yake bado anasema hataacha kumwomba Mungu kwa kuwa bado anamini kila jambo lina wakati wake na majira yake yawezekana bado muda na wakati wa bwana kwa yeye kuitwa mama lakini ni moja,kati jaribu analolipitia yeye katika maisha yake ya ndoa ndani ya miaka 20 iliyopita hata sasa,maadam wewe nawe ni mwombaji ninachukua fulsa hii kukuomba tusaidiane kumwombea,ili Mungu baba afungue kila kifungo kilichofungwa na ibilisi shetani katika mfomo wake wa uzazi ukapate kufunguka ili dada yetu naye afanikiwe kutoka kwenye kilio na masimango toka kwa jamii inayomzunguka.Yawezekana nawe ni mmoja kati ya  wanawake wanao lia juu ya hali hii tushirikiane katika kumwomba Mungu bado inawezekana haijalishi ni muda gani umekaa bila kupata mtoto,pia yawezekana hata sio wewe unauhitaji wa mtoto ila kuna mtu yeyote unayemfahamu kuwa anauhitaji mkubwa wa mtoto na amekuwa akipambana na ndugu wa mume wakitaka mtoto kwa hali yoyote.Poleni sana wadada na wamama ambao mnapita katika hali hii tuendelee kuombeana Mungu anasikia na anajua ni nini munahitaji toka kwake.Kama nawe unapenda kunishirikisha katika hitaji lako waweza nisikiliza katika Praise Power   Redio 99.2 fm kila siku kuanzia saa nane kamili usiku,au unaweza nipigia simu no              0715 408566.

Rafiki bado ninakuombea Mungu akubariki
Pamoja kwa Umoja

No comments:

Post a Comment

ABEDDY NGOSSO/SARA K

FANUEL SEDEKIA NA UPENDO WA YESU-MUNGU AKUBARIKI