KARIBU

KARIBU UPATE HABARI MBALIMBALI KUPITIA BLOG HII;;pamojakwaumoja2012.blogspot.com.
AU PIGA simu 0715408566 kwa Ushauri na maoni

KAULI MBIU/SLGN


HOPES

Thursday, August 9, 2012

DARASA HURU LA UFAHAMU.

  NINI HUTOKEA KWA MKE KUFIWA NA MUME AU MUME KUFIWA NA MKE AU WAPENZI MMOJA KUFA!!

  Jambo la kwanza linalohuzunisha zaidi ambalo lina kiwango cha asilimia 100 ni mtu kufiwa na mke au mume. Rekodi zinaonesha kuwa, watu wanaofiwa na wapenzi wao huwa na huzuni kubwa kiasi cha kutishia maisha yao.

Msongo wa mawazo, mauzauza ni mambo ambayo yanatajwa kusababisha vifo vya ghafla na vya muda mfupi kwa watu waliofiwa na waume/wake zao, huku sababu ya vifo hivyo ikibaki kuwa ni msongo wa mawazo (stress).

Licha ya ukweli kwamba kufiwa mume/mke ni jambo zito lakini, huzuni inapokuwa ya kudumu kiasi cha kutishia maisha ya mtu, suala la uzembe wa kufikiri huchukua nafasi. Hivyo, ili mtu aweze kuepukana na matatizo yanayotokana na kufiwa ni lazima afuate muongozo ufuatao ambao utamsaidia kuipunguza au kuiondoa huzuni hiyo ambayo ni mbaya kuliko nyingine zote duniani. Kwanza, ni kukubaliana na ukweli kwamba mwenza amefariki na hatarudi, kulia na kuhuzunika hakusaidii. Pili ni kuziondoa taratibu kumbukumbu zote zinazokuja na kutawala mawazo kuhusu mkeo/mumeo aliyekufa. Usiyazamishe mawazo kwenye tukio hilo, ukiona kuwaza kunajitokeza ni bora kupuuza mawazo hayo kwa kutoyapa nafasi ya kukutawala. Usipende kukaa peke yako kwa muda mrefu. Usiangalie picha na kutembelea kaburi la marehemu mara kwa mara bila kuwa na sababu za msingi. Usivute taswira ya maisha mliyokuwa mkiishi zamani. Kaa karibu na watu uwapendao, tembelea sehemu zenye kuvutia. Epuka kuzungumzia mambo ya marehemu wako. Badili mazingira ya chumba mlichokuwa mkilala, kuwa bize na majukumu yako na andaa mipango ya kumtafuta mwenza mpya,
Yote kwa yote mpe Mungu nafasi zaidi ili kuyaepuka madhara yasije kukupata katika kuamua na kuchagua akufaae katika maisha yako

Rafiki bado nakuombea Mungu akubariki
PAMOJA kwa UMOJA

No comments:

Post a Comment

ABEDDY NGOSSO/SARA K

FANUEL SEDEKIA NA UPENDO WA YESU-MUNGU AKUBARIKI