KARIBU

KARIBU UPATE HABARI MBALIMBALI KUPITIA BLOG HII;;pamojakwaumoja2012.blogspot.com.
AU PIGA simu 0715408566 kwa Ushauri na maoni

KAULI MBIU/SLGN


HOPES

Thursday, August 9, 2012

JE WAMTAMBUA NEYMA MUZYA MGAWE


YESU MTENDA MIUJIZA ANAZIDI KUTENDA MIUJIZA KILA ITWAPO LEO;;
BAADA YA KUPONA KATIKA AJALI YA PIKIPIKI NEYMA MGAWE MUNGU AMEWEZA KUMPA HUDUMA NA MAONO YA UIMBAJI NA SASA ANA NYIMBO AMEIMBA ILI KUKUONYESHA MUNGU ANAWEZA.
Huyu ndiye Neyma Mgawe akifurahia wema wa Mungu
Neyma Mgawe ndani vya viwanja Mlimani City.
Ndugu zangu naomba mnipokee katika huduma yangu hii ya uimbaji
KWA MAELEZO YAKE NEYMA MGAWE ANASEMA;;
Alianza kuimba akiwa bado mdogo na baada ya kusafiri kwenda kutembea Arusha kwa kaka yake Mungu alimpa kibali cha kuingia studio na kuimba nyimbo mbili ya kwanza ni Tenda muujiza na nyingine ni Mungu wa upendo.Anapendelea sana kuimba nyimbo za taratibu hasa za kuabudu,anapenda sana uimbaji wake ni Ephaim Sekeleti toka nchi Zambia.Neno ambalo alilopenda kuwaasa vijana wenzake anasema tumtafute Mungu maadam anapatikana pia tuache dhambi,anachukizwa sana na mavazi mabaya ambayo yanavaliwa na wadada wenzake.Wito wake kwa walio na vipaji basi wajaribu  kumwimbia yeye hata kama wanapita katika mapito magumu.Kuhusu albam yake anasema muda si mrefu na inawezekana kabla ya mwisho wa mwaka itakuwa tayari.Mwisho anasema anawatakia kila la kheri wadau wote wa  pamojakwaumoja2012.blogspot.com
Anatoka Mlandizi katika huduma ya KLPT Kisima cha Uzima


Rafiki bado nakuombea Mungu akubariki
PAMOJA kwa UMOJA

No comments:

Post a Comment

ABEDDY NGOSSO/SARA K

FANUEL SEDEKIA NA UPENDO WA YESU-MUNGU AKUBARIKI