KARIBU

KARIBU UPATE HABARI MBALIMBALI KUPITIA BLOG HII;;pamojakwaumoja2012.blogspot.com.
AU PIGA simu 0715408566 kwa Ushauri na maoni

KAULI MBIU/SLGN


HOPES

Friday, November 2, 2012

SAFARI YA MSAFIRI IKOJE NA NINI KUSUDI LA MUNGU

TUNAJIFUNZA NINI KATIKA UWINGI WA MATUKIO KAMA HAYA KATIKA SAFARI YA MSAFIRI
 Bonyeza play uimbe wimbo huu wa MAHARI NI PAZURI




















Tuna kila sababu ya kujihoji juu ya haya yote japo sio lahisi kuelewa nini nina maanisha,lakini jiulize nini chanzo maana ukishaelewa chanzo utajua mengi katika safari ya msafiri ambaye ni mimi na wewe.
Wakati mwingine tumeshindwa kujiuliza kwa kuwa ndiyo maisha yetu na tumekuwa wakali sana pale anapotokea mtu akazungumzia jambo linalo refrect maisha yako,hali hii imefika hata makanisani leo hii wachungaji wameshindwa kusema ukweli kwa kulinda watu kukimbia makanisa yao.Swali langu nini  misingi ya kanisa na nani mlengwa hasa mpaka imefika wakati kanisa limeshindwa kusema ukweli kwa kuhofia watu kuhama kwasababu ya kuhubiri au kufundisha ukweli,Je hawa tunaowaona wana athirika na mateso ya shetani ndiyo waathirika wa waliokimbia makanisa kwa kuambiwa ukweli au ni nini basi kinatokea katika safari ya msafiri.
Maswali ya kujiuliza yako mengi ikiwa ni pamoja na nini chanzo cha watu kupoteza upendo na subira katika maisha yao,nikwasababu Yesu amechelewa kuja au nini,sitaki kuamini maisha ni magumu sana hata kuwa ndiyo chanzo cha kutokuwepo na upendo.
Hivi watu wamesahau yakuwa kuuwa ni dhambi na kujiuwa ni dhambi vile vile,hizi roho za hawa zinapokuwa zinalia zinamlilia nani aliyeziumba au anayezihukumu??
Kijana ambaye umepewa akili yenye kutambua jema na baya kwanini kuangamia kwa kukosa maarifa?
Kanisa la Mungu la leo liko wapi haya yote yanatokea kila siku bila kupungua tena kwa kasi zaidi?
Je hili ndilo kusudi la Mungu juu ya safari ya msafiri hapa Duniani?
TAFAKARI:
MUNGU ANA SABABU NA UHAI WAKO SANA JIULIZE MASWALI MENGI JUU KILA KINACHOTOKEA LEO,NINI SABABU YA HALI HII 1. UMASIKINI 2.HOFU YA MUNGU KUTOWEKA KWA WATU 3.KUKATA TAMAA.......Tafakari sana hali hii nani mkosa kati ya huyu au aliyekatisha maisha ya huyu.Kumbuka sisi sote ni watoto wa baba moja na yatupasa kupendana na kuchukuliana madhaifu. 
Ndugu yangu kila mmoja wetu asimame katika nafasi yake kuomba ili safari ya msafiri ilifikie kusudi la Mungu
Kwanza samahani kwa picha hizi ulizoziona hapa juu ila jiulize kwanini Mungu kakupa wewe nafasi ya kuziona na si mtu mwingine!!!! MUNGU ana makusudi na wewe .
Yawezekana ndani mwako amani imetoweka kwa na unataka kutubu mbele za Mungu na sasa uko tayari kuongozwa sala ya toba:
Bonyeza hapa play hapa chini kisha fuata maneno utakayo yasikia.

Rafiki bado nakuombea Mungu akubariki
PAMOJA kwa UMOJA

No comments:

Post a Comment

ABEDDY NGOSSO/SARA K

FANUEL SEDEKIA NA UPENDO WA YESU-MUNGU AKUBARIKI