KARIBU

KARIBU UPATE HABARI MBALIMBALI KUPITIA BLOG HII;;pamojakwaumoja2012.blogspot.com.
AU PIGA simu 0715408566 kwa Ushauri na maoni

KAULI MBIU/SLGN


HOPES

Monday, July 30, 2012

GAFLA BAHATI BUKUKU AANZA KUFANYA VYEMA BAADA YA KUTOA NYIMBO MPYA

BAHATI BUKUKU AMETEKA HISIA ZA WASIKILIZAJI WENGI HASA ZA WANAWAKE  BAADA YA KUTOA NYIMBO MPYA IJULIKANAYO DUNIA HAINA HURUMA.
Bahati Bukuku kama anavyoonekena katika picha
Jana nilifanikiwa kuzungumza naye kwa njia ya simu na mazungumzo yalikuwa hivi

Hellow mtumishi wa Mungu bwana yesu asifiwe?
Amen" habari ya uzima kaka yangu?
Nzuri sana dada yangu habari za wapi tena mtumishi
Dah! nipo tu kaka yangu kwani vipi sipatikani hewani? eeti hellow??
Hapana sio kwamba haupatikani hewani naona hatuonani kama awali tulivyokuwa tunapishana mtaani
Hapana kaka yangu niko mkoani Kilimanjaro ndiyo maana hatuonani.
Okey ndiyo maana sikuoni nilikuwa nadhani uko location kwa ajili ya Filamu.
Hapana!! ishu ya filamu bado ila bado nina pokea maombi ya watu wanaotaka kuwa katika filamu hii
Okey!!Aiseee Kilimanjaro nasi Mwanza ambako ulikuwa wiki iliyopita?
Kaka yangu we acha tu!! niko Kilimanjaro tena ndani ndani huku! Mungu anasaidia huduma inawafikia watu.
Dah!! umeongea kuhusu Moshi umenikumbusha maeneo ya Bomang'ombe.
Hahahahahahaha!!! nilipita juzi nikitokea maeneo ya Sanya juu!.
Hahahahaha!! dah! si utani kazi ya bwana inasonga mbele.
Okey tuachane na hayo niambie unajisikiaje watu walivyoipokea kazi yako mpya 
Hakika nazidi kumshang'aa sana huyu 
Mungu jinsi ambavyo anazidi kunitendea juu ya kazi hii mpya tayari huwezi kuamini kaka yangu  nimeshaitwa sehemu nyingi sana  nimebaki najiuliza wameisika wapi wakati ina muda mchache hewani.
Dada acha Mungu aitwe Mungu kwani yeye ndiye muweza wa yote maadam umemuimbia yeye hili ndilo jibu watu wanapata kuhudumiwa kupitia nyimbo zako so Mungu hawezi kaaa kimya juu ya ujumbe wake kuwafikia watu wake.
Ni kweli kaka yangu nakubaliana na wewe kwa usemi huo!
Jana nilikuwa nazungumza na mmoja kati ya msikilizaji wa redio aliniambia umemgusa maisha yake na tena anaomba kama itawezekana iigize katika filamu hii kwa maan ani maisha yake halisi yaliyo katika wimbo wako.!
Weweee! kweli anasema kila kitu nilichokiimba humo ndiyo maisha yake halisi
Yeah!! asilimia kubwa ni sehemu ya maisha yake halisi.
Mtumishi ya kuongea yako mengii la ngoja nikuache na mimi niendelee na maandalizi ya kipindi cha usiku(Kesha na PPR).
Okey kaka kila lakheri tutaonana kati ya jumatatu nikitoka Moshi,pia na mimi ngoja nijiandae maana napanda jukwaani muda si mrefu.
Ok barikiwa sana pia huduma njema!
Haya kaka yangu mungu akubariki sana wewe na watangazaji wenzako wote hapo!sorry nasiki kama nyimbo yangu hewani??
Yeah!! hahahaha! iko hewani siunajua watu wameipenda.
bye byeeeee!!!! 
Haya ndiyo yalikuwa mazungumzo kati yangu na Dada Bahati Bukuku akiwa Kilimanjaro(Moshi).

Rafiki bado nakuombea Mungu akubariki
Pamoja kwa Umoja

No comments:

Post a Comment

ABEDDY NGOSSO/SARA K

FANUEL SEDEKIA NA UPENDO WA YESU-MUNGU AKUBARIKI